Patagonia ni sehemu ya kusini kabisa ya bara la Amerika ya Kusini yenye umbo la pembetatu ndefu. Inajumlisha sehemu za kusini za Argentina na Chile. Iko kusini kwa mto Río Colorado ya Argentina na mto Río Bío Bío ya Chile. Upande wa magharibi iko bahari ya Pasifiki na upande wa mashariki ile ya Atlantiki zinazokutana kusini kabisa katika mlangobahari wa Magellan. Kusini kwa mlango bahari huo liko funguvisiwa la Tierra del Fuego (nchi ya moto).

Rangi ya njano inaonyesha eneo la Patagonia.

Mikoa ya Chile ya Los Lagos, Aysen na Magallanes pamoja na mikoa ya Argentina ya Neuquén, Río Negro, Chubut, Santa Cruz na Tierra del Fuego katika Mkoa wa Tierra del Fuego, Antaktiki na Visiwa vya Atlantiki Kusini iko yote katika Patagonia.

Wakazi na eneo hariri

  • Wakazi = 1,740,000 (sensa ya mwaka 2001).
  • Eneo = km² 900,000 pamoja na Patagonia ya Chile na Tierra del Fuego
  • Msongamano wa watu = 2.21 / km²

Jiografia hariri

Sehemu kubwa ya Patagonia ya Argentina ni tambarare kavu kwa sababu mvua haipiti milima ya Andes. Hali ya hewa ni baridi kiasi hadi baridi.

Patagonia ya Chile inapokea mvua nyingi mlimani. Kusini penye baridi kuna barafuto kubwa.

Uchumi hariri

Migodi na uvuvi baharini ni muhimu. Katika nchi kavu ya kusini kuna ufugaji wa kondoo. Kaskazini kuna kilimo.

Picha hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika Kusini bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Patagonia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.