Pierce Brendan Brosnan (amezaliwa 16 Mei 1953, Drogheda, Ireland) ni mwigizaji filamu na mtaarishaji wa Kiireland-Marekani. Labda anafahamika zaidi kwa kuigiza kama 'James Bond' katika filamu nne alizocheza kuanzia mwaka 1995 hadi 2002, ambazo ni GoldenEye, Tomorrow Never Dies, The World Is Not Enough na Die Another Day. Tangu atumie jina James bond Brosnan, pia amecheza filamu zingine tofauti ikiwemo ile ya "Evelyn" na "Seraphim Falls".

Pierce Brosnan

Bond kwenye Cannes Film Festival, 2002
Amezaliwa Pierce Brendan Brosnan
16 Mei 1953 (1953-05-16) (umri 70)
Navan, County Meath, Ireland
Kazi yake Mwigizaji, mtayarishaji
Miaka ya kazi 1979–hadi leo
Ndoa Cassandra Harris
(1977–1991) (kifo chake)
Keely Shaye Smith
(2001–hadi leo)
Tovuti rasmi

Pia Brosnan ana kampuni yake inayojishughulisha na maswala ya utengenezaji wa filamu, moja kati ya filamu walizotengeneza ni 'Butterfly on a Wheel, Mamma Mia! na The Topkapi Affair, toka mwaka 1999 alivyo anza ile filamu ya The Thomas Crown Affair.

Maisha ya awali hariri

Brosnan ni Mtoto wa pekee wa Thomas na May, alizaliwa Drogheda, County Louth, Ireland, Brosnan alipelekwa karibu kidogo na mji wa Navan, County Meath ambako huko ndiko alipo kuwa anasoma, alisoma katika shule flani ya kawaida iliyokuwa inaendeshwa na "De La Salle Brothers. Brosnan na Mama yake walihamia mjini London, Uingereza kwa ajili ya kazi baada ya baba yake kuitelekeza familia yake, mwaka 1964, bond alivyofika umri wa miaka kumi na moja baba yake aliirudia familia yake.

Kwa bahati mbaya mama yake akadai taraka, hivyo walikatarikiana na mama yake kuolewa na mzee wa kiingeza alyepigana Vita Kuu ya Pili ya Dunia mzee William Charmichael, ambaye alimlea Bond kama mwanae wa kumzaa yeye hali ya kuwa ni mtoto wa kufikia.

Charmichael alikuwa wa kwanza kumchukua brosnan na kumpeleka kutazama filamu za James Bond, filamu hiyo ilikuwa ile ya "Gold Finger". Brosnan alisoma katika shule ya 'The Elliot School' ya mjini London, baadae 'secondary modern school', Putney, ilyopo magharibi mwa mji wa London. Brosnan alikuwa na mahusiano ya karibu sana na mwalimu wake wa Jiografia wakati yupo shule anasoma. Alivyomaliza shule jina lake la utani likuwa 'Irish'.

Baada ya masomo Brosnan alitamani sana kuwa msaniii na ndipo alipo anza maelekezo hayo kibiashara katika chuo cha "Central Saint Martins College of Art and Design. Alivyofika umri wa miaka 16 wakala wa sarakasi alimuona Brosnan akachezea moto huku akifanya kama ana ula wakala huyo aka mkodi Brosnan. Baadae alipata mafunzo ya sanaa kwa muda wa miaka mitatu katika chuo cha "The Drama Centre" cha mjini London Uingereza.

Maisha binafsi hariri

Brosnan alimuoa muigizaji filamu wa Kiaustralia "Cassandra Harris" hiyo ilikuwa mwaka 1980 na kumlelea watoto wake wawili, ambaye ni Charlotte,(alyezaliwa, 1971) na Christopher (Aliyezaliwa, 1972) kwa bahati mbaya baba yao alikuja kufa hiyo ilikuwa mnamo mwaka 1986.

Brosnan na Harris walizaa mtoto mmoja wa kiume aliyeitwa "Sean" (Alizaliwa, 1983). Ilivyofika mwaka 1991 Harris alifariki dunia kwa ugonjwa wa Saratani, Miaka kumi na Moja toka waoane.

Mwaka 2001 Brosnan akamuoa Mwandishi wa habari wa kimarekani Keely Shaye Smith, Wamezaa watoto wawili wa Kiume Mmoja Dylan Thomas (Aliz. 1997) na mwingine Paris Beckett (Aliz. 2001).

Tarehe 23 Septemba 2004, Brosnan amekuwa raia wa marekani, na kwa sasa anaishi mjini Malibu, California na ana nyumba mjini Hawaii na Kaskazini mwa Dublin nchini Uingereza.

Filamu alizoigiza hariri

  • The Long Good Friday (1980)
  • The Mirror Crack'd (1980)
  • Nomads (1986)
  • Taffin (1987)
  • The Fourth Protocol (1987)
  • The Deceivers (1988)
  • Noble House (1988)
  • Around the World in Eighty (1989)
  • Mister Johnson (1990)
  • The Lawnmower Man (1992)
  • Live Wire (1992)
  • Mrs. Doubtfire(1993)
  • Death Train(1993)
  • Love Affair (1994)
  • Night Watch (1995)
  • GoldenEye (1995)
  • Mars Attacks (1996)
  • The Mirror Has Two Faces (1996)
  • Robinson Crusoe The Movie (1997)
  • Tomorrow Never Dies (1997)
  • Dante's Peak (1997)
  • Quest for Camelot (1998)
  • Grey Owl (1999)
  • The World Is Not Enough (1999)
  • The Thomas Crown Affair (1999)
  • The Tailor of Panama (2001)
  • Die Another Day (2002)
  • Evelyn (2002)
  • After the Sunset (2004)
  • Laws of Attraction (2004)
  • The Matador (2005)
  • Seraphim Falls (2007)
  • Butterfly on a Wheel (2007)
  • Married Life (2007)
  • The Topkapi Affair (2008)
  • Mamma Mia (2008)
  • Caitlin (2008)
  • The Greatest (2009)
  • The Ghost Writer (2010)
  • Remember Me (2010)
  • Oceans (2010)
  • Salvation Boulevard (2011)
  • I Don't Know How She Does It (2011)
  • Bag of Bones (2011)
  • Love Is All You Need (2013)
  • The World's End (2013)
  • The Love Punch (2014)
  • A Long Way Dow (2014)
  • The November Man (2014)
  • Some Kind of Beautiful (2015)
  • Survivor (2015)
  • No Escape (2015)
  • Urge (2015)
  • The Moon and The Sun

Viungo vya nje hariri

 
WikiMedia Commons