Pirenei (Kifaransa: Pyrénées; Kihispania: Pirineos) ni safu ya milima katika Ulaya ya kusini-magharibi inayotenganisha nchi za Ufaransa na Hispania. Zina urefu wa kilomita 430 kati ya bahari ya Atlantiki na bahari ya Mediteranea.

Pirenei za kati zinavyoonekana kutoka Pic du Midi de Bigorre
Pirenei wakati wa kiangazi

Pirenei za kati ni sehemu ya juu kuna milima 200 yenye kimo cha zaidi ya mita 3000. Mingi ina barafu na theluji ya kudumu hata kama barafuto zinarudi nyuma. Milima mikubwa ni hasa

  • Pico d'Aneto au Pic de Néthou yenye mita 3,404
  • Mont Posets yenye mita 3,375
  • Mont Perdu au Monte Perdido au Mont Perdut ("mlima uliopotea") 3,355 m (11,007 ft).

Katika historia Pirenei zilikuwa kizuizi cha usafiri hivyo pia mpaka muhimu wa kisiasa. Mipito ni michache tena mikali. Katikati ya milima iko utemi wa Andorra iliyobaki kama nchi ya pekee kwa sababu ya tabia ya milima iliyozuia nchi kubwa jirani zisiimeze.

Tovuti za Nje hariri

 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Pirenei kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.