Porto Novo (Kireno kwa: "Bandari mpya" - inaitwa na wenyeji pia Hogbonou na Adjache) ni mji mkuu rasmi wa Benin. Ni mji wa bandari kwenye kidaka cha Atlantiki.

Jiji la Porto Novo
Nchi Benin
Sehemu ya Mji wa Porto Novo
Porto Novo - ramani ya mji
Porto Novo katika Benin

Mwaka 2002 Porto Novo ilikuwa na wakazi 223,552 (sensa 2002) na mji wa pili katika Benin. Hapa ni ikulu ya rais na makao ya bunge lakini wizara nyingi zina ofisi zao mjini Cotonou.

Historia hariri

Jina la kihistoria ni Ajache. Kwa jina hili mji ulikuwa mji mkuu wa ufalme wa Aja. Wareno walijenga kituo cha biashara ya watumwa wakaiita "Porto Novo - bandari mpya". Mwaka 1863 ufalme ulikubali ulinzi wa Ufaransa kwa hofu ya Waingerezea. 1883 eneo lake likawa sehemu ya koloni ya Kifaransa ya Dahomey na mwaka 1900 mji mkuuw a koloni yote.

Wafalme wa Porto Novo waliendelea kuwa na makao mjini hadi kifo cha mfalme wa mwisho Alohinto Gbeffa mwaka 1976.

Tangu mwisho wa utumwa huko Brazil Waafrika wa Brazil walirudi wakifika Porto Novo na kukaa hapa. Hivyo athira za Brazil zimeonekana katika utamaduni wa mji, hasa katika ujenzi na chakula.

Viungo vya Nje hariri