Pyotr Leonidovich Kapitsa (8 Julai 18948 Aprili 1984) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Urusi. Hasa alichunguza nadharia ya usumaku. Alifanya kazi nchini Uingereza pamoja na Ernest Rutherford kuanzia mwaka wa 1921 hadi 1934 alipolazimishwa na Yosip Stalin kubaki Urusi kama mkurugenzi wa utafiti wa fizikia. Mwaka wa 1978, pamoja na Arno Penzias na Robert Woodrow Wilson alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.

mchoro wa Kapitsa (upande wa kushoto) ulivyochorwa na Boris Kustodiyev


Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Pyotr Kapitsa kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.