Quincy Delight Jones, Jr. (amezaliwa tar. 14 Machi 1933) ni mwelekezi wa muziki, mtayarishaji wa rekodi, mpangaji muziki, mtunzi wa vibwagizo vya filamu, na mpiga talumbeta kutoka nchini Marekani. Katika kipindi cha makumi yake matatu ya shughuli za kiburudani, Jones amepata kushindanishwa katika tuzo za Grammy Award mara 79,[1] kashinda 27 Grammys,[1] ikiwemo na tuzo ya Grammy Legend Award mnamo 1991. Anafahamika zaidi na zaidi kwa kutayarisha albamu ya Thriller, ya mwanamuziki wa pop Michael Jackson, ambayo imeuza zaidi ya nakala milioni 110 dunia nzima,[2] na ndiyo mtayarishaji na mwelekezi wa wimbo wa hisani wa “We Are the World”.

Quincy Jones
Quincy Jones mnamo 2014
Quincy Jones mnamo 2014
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Quincy Delight Jones, Jr.
Amezaliwa 14 Machi 1933 (1933-03-14) (umri 91)
Chicago, Illinois
Asili yake Seattle, Washington
Aina ya muziki Pop, funk, soul, big band, swing, jazz, traditional pop, bossa nova
Kazi yake Mwanamuziki, mwelekezi, mtayarishaji, mpangaji, mutunzi,
Miaka ya kazi 1951 – hadi leo
Studio Columbia, Mercury, Qwest
Ame/Wameshirikiana na Michael Jackson, Frank Sinatra, Dinah Washington, Dean Martin, Patti Austin, Tevin Campbell, Marvin Gaye, Stevie Wonder, Will Smith
Tovuti Official Quincy Jones Website

Huyu pia anajulikana kwa kazi yake ya 1962 wimbo "Soul Bossa Nova", ambayo ilikuwa na asili kamili ya albamu ya Big Band Bossa Nova. "Soul Bossa Nova" ulikuwa wimbo uliochaguliwa na kutumiwa kwenye Kombe la Dunia la mwaka 1998, kipindi cha Kikanada cha Definition, filamu ya Woody Allen Take the Money and Run na Mike Myers, Austin Powers: International Man of Mystery, na pia ushawihi kusampuliwa na kikundi cha hip hop cha Kikanada Dream Warriors kwa ajili ya wimbo wao wa "My Definition of a Boombastic Jazz Style".

Mnamo mwaka wa 1968, Jones na mtunzi wa nyimbo mwenzake Bw. Bob Russell wamekuwa ndiyo Waafrika-Waamerika wa kwanza kushindanishwa kwenye tuzo za Academy Award katika kundi la "Nyimbo Bora za Asilia". Mwaka huohuo, amekuwa Mwafrika-Mwamerika wa kwanza kuchaguliwa mara mbili katika kipindi cha mwaka mmoja kwa kazi yake ya kutengeneza kibwagizo cha filamu ya mwaka wa 1967, In Cold Blood.

Mnamo mwaka wa 1971 Jones angepokea taji la heshima na kuwa Mwafrika-Mwamwerika wa kwanza kupewa jina la kiongozi wa muziki/mwelekezi wa sherehe za Academy Awards. Jones pia alikuwa wa kwanza (na mpaka sasa, ni yeye pekee) Mwafrika-Mwamerika kuchaguliwa kuwa kama mtayarishaji katika kundi la Filamu Bora (mnamo 1986, kwa ajili ya The Color Purple).

Wasifu hariri

Maisha ya awali hariri

Jones alizaliwa mjini Chicago, akiwa kama mtoto mkubwa wa Bi. Sarah Frances, meneja wa majengo na makazi na pia ni mkurugenzi wa benki ambaye alisumbuliwa na skizofrenia, na Quincy Delight Jones, Sr., mchezaji wa kulipwa wa baseball na pia selemala.[3] Jones aligundua masuala ya muziki akiwa katika shule ya Raymond Elementary School iliyo huko mjini Kusini mwa Chicago na kujifunza talumbeta. Alipokuwa na umri wa miaka ya 10, familia yake ikahamia mjini Bremerton, Washington na kwenda kujiunga na shule ya mjini Seattle Garfield High School. Baadaye akajiunga na Somerset Academy.

Mnamo mwaka wa 1951, Jones amepata udhamini kwa kwenda kujifua zaidi kimasomo ya muziki, Schillinger House ya mjni Boston, Massachusetts. Lakini, alitelekeza masomo na kupokewa ofa ya kwenda kwenye ziara moja aliyokuwa kama mpiga talumbeta wa kiongozi wa bendi Bw. Lionel Hampton. Baadaye Jones akaelekea zake mjini New York City, ambap alipata bahari kadhaa za kuwaandalia muziki baadhi ya wasanii kama vile Sarah Vaughan, Dinah Washington, Count Basie, Duke Ellington, Gene Krupa, na rafiki yake wa karibu Ray Charles.

Shughuli za muziki hariri

Kufanyakazi na Michael Jackson hariri

Wakati anasghulikia filamu ya The Wiz, Michael Jackson akamwomba Jones amtayarishie albamu yake ijayo ya kujitegemea. Jibu lake likawa, Off the Wall iliyouza nakala milioni 20 na kumfanya Jones kuwa mtayarishaji mkubwa na mwenye nguvu katika soko la muziki. Jones na Jackson wakashirkiana na tena kutengeneza albamu ya Thriller iliyofanya mauzo ya heshima kwa nakala milioni 110 kwa hesabu ya dunia nzima na kuifanya iwe albamu yenye mauzo bora kwa muda wote (miaka nenda miaka rudi).[4] Jones akafanyakazi tena na Michael Jackson kwenye albamu yake ya tatu ya Bad, ambayo iliuza nakala milioni 32. Baada ya albamu ya Bad, Jones akamtaka Jackson aende kwa waanzilishi wa New Jack Swing Bw. Teddy Riley na Babyface hivyo Jackson anaweza "kubadili" sauti yake zaidi.

Katika mahojiano mnamo mwaka wa 2002, pale Jackson alipoulizwa kama angeweza kufanyakazi tena Jones alijibu, "mlango uko wazi muda wote". Hata hivyo, mnamo mwaka 2007, pale NME.COM walivyomuuliza Jones swali lilelile, alisema "Bwana tafadhali, nina mengi ya kufanya. Tulishafanya hivyo tayari. Nimezungumza naye kuhusu kufanya naye kazi tena, lakini nina mengi mno ya kufanya. Nina shughuli zaidi ya 900, na nina umri wa miaka 74. Hebu nipumzisheni".[5]

Kwa kufuatia kifo cha Jackson mnamo tar. 25 Juni 2009, Jones alisema:

Yaani nimevurgwa kabisa na msiba huu na ni habari sizo za kutarajia. Kwa Michael kuchukuliwa kwetu ghafula hivyo akiwa na umri mdogo kama ule, wala sina la kusema. Ni mapenzi ya Mungu tu yaliyoleta nafsi zetu pamoja na kufanyakazi katika The Wiz na kuturuhusu kufanya kile tulichotakiwa kukifanya kwa miaka ya 1980. Kwa siku hizi, muziki tulioumba pamoja katika Off The Wall, Thriller na Bad unapigwa katika kila kona ya dunia na sababu ya hiyo ni kwa sababu ndicho alichojaaliwa...kipaji, hekima, utaaluma na kupea umuhimu kwa wetu wengine. Alikuwa mburudishaji aliyetimia na michango yake na urithi wake utabaki ukikumbukwa duniani milele na milele. Leo hii nimempoteza mdogo wangu jamani, na sehemu ya nafsi yangu imeondoka na yeye.

Kufanyakazi na Frank Sinatra hariri

Maisha binafsi hariri

Diskografia hariri

Marejeo hariri

  1. 1.0 1.1 Callaway, Sue (2007-01-28). Fortune test drives a Mercedes Maybach with Quincy Jones — February 5, 2007. Money.cnn.com. Iliwekwa mnamo 2009-07-18.
  2. Jacko's Back! | MTV UK. Mtv.co.uk (2006-11-16). Jalada kutoka ya awali juu ya 2007-09-30. Iliwekwa mnamo 2009-07-18.
  3. Quincy Jones Biography (1933-). Filmreference.com. Iliwekwa mnamo 2009-07-18.
  4. [1]
  5. Quincy Jones snubs chance to team up with Michael Jackson | News | NME.COM. Nme.Com<! (2007-05-25). Iliwekwa mnamo 2009-07-18.

Viungo vya nje hariri

 
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


  Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Marekani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Quincy Jones kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.