Rashidi Yekini (23 Oktoba 19634 Mei 2012) alikuwa mchezaji wa mpira wa miguu aliyetumikia kama mshambuliaji timu ya taifa ya Nigeria.

Rashidi Yekini
Maelezo binafsi
Jina kamili Rashidi Yekini
Tarehe ya kuzaliwa (1963-10-23)Oktoba 23, 1963
Mahala pa kuzaliwa    Kaduna, Nigeria
Tarehe ya kufa    4 Mei 2012 (umri 48)
Mahala alipo fia    Ibadan, Nigeria
Urefu 1.90m
Nafasi anayochezea Mshambulizi
Maelezo ya klabu
Klabu ya sasa Amestaafu
Klabu za ukubwani
Miaka Klabu
1981–1982
1982–1984
1984–1987
1987–1990
1990–1994
1994–1995
1995–1996
1997
1997–1998
1998–1999
1999
1999–2002
2002–2003
2005
UNTL Kaduna
Shooting Stars
Abiola Babes
Africa Sports
Vitória Setúbal
Olympiacos
Sporting Gijón
Vitória Setúbal
FC Zürich
Bizerte
Al-Shabab
Africa Sports
Julius Berger
Gateway
Timu ya taifa
1986–1998 Nigeria

* Magoli alioshinda

Wasifu wa Klabu hariri

Baada ya kuanza kucheza kandanda katika Ligi ya Nigeria, Yekini alihamia Côte d'Ivoire kucheza [1] katika timu ya Africa Sports National. Kutoka hapo,alihamia timu ya Vitória de Setúbal ya Ureno, alipofanikiwa sana na kupata miaka mizuri katika kandanda. Hatimaye, alikuwa mwanakandanda mwenye mabao nyingi sana katika ligi ya Ureno ya daraja la kwanza katika msimu wa 1993-1994. Utendaji wake katika mwaka huo ulimpa tuzo ya Mwanakandanda bora wa Afrika katika mwaka wa 1993, wa kwanza kabisa kutoka taifa lake.

Baada ya Shindano la Kombe la Dunia la 1994,Yekini aliajiriwa na klabu ya OLympiacos CFP lakini hakuelewana na wenzake katika timu.Hivyo basi, akakusanya virago vyake na kutoka timu hiyo. Tangu hapo, kazi yake ya uchezaji haikunawiri tena hata aliporudi Vitória de Setúbal. Alicheza katika timu za FC Zürich, Club Athlétique Bizertin na Al-Shabab (Saudi Arabia), kabla ya kurejea Africa Sports National. Katika mwaka wa 2003, Yekini, akiwa umri wa miaka 39, alirudi katika Ligi ya Mabingwa wa Nigeria akicheza katika klabu ya Julius Berger.

Katika mwaka wa 2005, akiwa umri wa miaka 41,Yekini alirudi kucheza kwa muda mfupi akiwa pamoja na mwenzake aliyekuwa katika timu ya taifa pamoja,Mobi Oparaku.Walicheza katika klabu ya Gateway FC.

Wasifu wa Kimataifa hariri

Alifunga mabao 37 katika mechi 70 alizocheza akiwa timu ya taifa ya Nigeria.Hivi sasa ,bado yeye ndiye anayeshikilia rekodi ya mabao mengi katika timu ya taifa ya Nigeria. Alikuwa katika timu iliyohusika katika Shindano la Kombe la Dunia la 1994 na Shindano la Kombe la Dunia la 1998.Katika Shindano hilo la 1994, alifunga bao la kwanza la Nigeria kabisa katika Kombe la Dunia la FIFA katika ushindi wao wa 3-0 dhidi ya Bulgaria.

Aidha,Yekini alisaidia Nigeria kushinda Kombe la Mataifa ya Afrika la 1994. Alikuwa amecheza katika michezo ya Olimpiki ya 1988 jijini Seoul.Yekini alifunga mabao mengi katika Kombe la Mataifa ya Afrika kuliko mwanakandanda mwingine katika shindano hilo.

Marejeo hariri

  1. Yakubu ni wa Nigeria

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rashidi Yekini kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.