"Ready or Not" ni single ya pili kutoka kwa kundi zima la muziki wa hip hop The Fugees. Wimbo ulitoka mwaka wa 1996 kutoka katika albamu ya The Score. Wimbo umechukua sampuli ya wimbo wa "Boadicea" wa Enya, na kiitikio chake kinatokana na wimbo wa "Ready or Not Here I Come (Can't Hide from Love)" wa The Delfonics. Wimbo ulitumia majuma mawili kwenye chati za UK Singles Chart mnamo mwezi wa Septemba katika mwaka wa 1996.[1]

“Ready or Not”
“Ready or Not” cover
Single ya The Fugees
kutoka katika albamu ya The Score
Imetolewa 2 Septemba 1996
Muundo CD single, 12" single
Imerekodiwa 1995
Aina Hip hop
Urefu 3:47
Studio Ruffhouse Records
Mtunzi Nelust Wyclef Jean
Samuel Prakazrel Michel
Lauryn Hill
William Hart
Thom Bell
Mtayarishaji Wyclef, Lauryn Hill, Prakazrel "Pras" (co-producer), Jerry 'Wonder' Duplessis (co-producer)
Mwenendo wa single za The Fugees
"Fu-Gee-La"
(1996)
"Ready or Not"
(1996)
"No Woman, No Cry"
(1996)

Mwimbaji Enya alipanga kulishtaki kundi hili kwa sababu za ukiukwaji wa hakimiliki, kwa sababu hajaruhusu kundi la The Fugees kuchukua sampuli ya wimbo wake wa "Boadicea", kutoka katika albamu ya mwaka wa 1992, The Celts.[2] Hatimaye mpango mzima ukasawazishwa huko mahakamani.

Wimbo ulikuja kurudiwa tena na msanii wa muziki wa house wa Ulaya The Course mnamo mwaka wa 1997. Ulifikia nafasi ya #5 nchini Uingereza kwa mwezi wa Aprili katika mwaka huo.[3]

Rais wa Marekani Barack Obama ameuita "Ready or Not" kama wimbo wake kipenzi kutoka katika orodha ya 10 bora iliyotolewa na Blender mnamo mwezoi wa Agosti katika mwaka wa 2008.[4]

Orodha ya nyimbo hariri

CD1 hariri

  1. "Ready Or Not" (Radio Version) - 3:47
  2. "Ready Or Not" (Salaam's Ready For The Show Remix) - 4:24
  3. "Ready Or Not" (Handel's Yaard Vibe Mix) - 4:41
  4. "The Score" - 4:32

CD2 hariri

  1. "Ready Or Not" (Album Version) - 3:50
  2. "How Many Mics" - 4:23
  3. "Freestyle" - 5:03
  4. "Blame It On The Sun" - 5:41

Marejeo hariri

  1. The Fugees UK chart info Chartstats.com. Retrieved 23 Mei 2009.
  2. Irish Voice article at archive.org (1997-02-18). Jalada kutoka ya awali juu ya 2005-04-07. Iliwekwa mnamo 2007-03-26.
  3. The Course UK chart info Chartstats.com. Retrieved 23 Mei 2009.
  4. White House DJ Battle. Blender Magazine. Jalada kutoka ya awali juu ya 2009-04-27. Iliwekwa mnamo 2008-08-04.