Rudesindo (pia: Rosendo; Santo Tirso, Ureno, 26 Novemba 907 - Celanova, Hispania, 1 Machi 977) alikuwa mapema mmonaki, akawa askofu wa Mondonyedo - Dumio akiwa na umri wa miaka 18 kuanzia 925 hadi 950, halafu 955-958, lakini pia gavana 955-969.

Sanamu ya Mt. Rudesindo.

Kati ya juhudi zake, kuna uanzishaji wa monasteri kadhaa na kuongoza jeshi dhidi ya wavamizi Waarabu na Wanormani.

Mwaka 968 hadi 977 alikabidhiwa jimbo lingine akawa abati wa Celanova, alipotembelewa na watu wengi kwa ajili ya ushauri[1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 1 Machi[2].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

  • Filippo Caraffa e Giuseppe Morelli (curr.), Bibliotheca Sanctorum (BSS), 12 voll., Istituto Giovanni XXIII nella Pontificia Università Lateranense, Roma 1961-1969.
  • Pio Paschini (cur.), Enciclopedia Cattolica (EC), 12 voll., Ente per l'Enciclopedia Cattolica e per il libro cattolico, Città del Vaticano 1948-1954.

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.