Ruth First

Mwanasiasa wa Afrika Kusini (1925-1982)

Ruth First (4 Mei 1925 - 17 Agosti 1982) alikuwa mwanaharakati na mwandishi wa Afrika Kusini. Mwaka wa 1963, kwa vile aliandika dhidi ya ubaguzi wa rangi alikamatwa na kutiwa ndani bila kesi. Alikuwa mhariri wa magazeti mbalimbali zilizopigwa marufuku, kama The Guardian, New Age na Fighting Talk. Alihamia Uingereza na baadaye Msumbiji ambapo alifundisha katika Chuo Kikuu cha Maputo. Aliuawa na bomu lililofichwa ndani ya kifurushi cha posta.

Ruth First
[[Image:|225px|alt=]]
Amezaliwa 4 Mei 1925
Johannesburg, Afrika Kusini
Amekufa 17 Agosti 1982
Msumbiji
Kazi yake Mwanaharakati, Mwandishi

Maandishi yake hariri

  • South West Africa (1963)
  • 117 Days (1965)
  • No Easy Walk to Freedom (1965, mhariri wa hotuba za Nelson Mandela)
  • Olive Schreiner (1980, wasifu pamoja na Ann Scott)

Angalia pia hariri

Viungo vya nje hariri

Marejeo hariri

  • Chapman, Michael. 2003. Southern African Literatures, University of Natal Press. ISBN 1-86914-028-1
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ruth First kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.