Samir Nasri

Mchezaji mpira wa Ufaransa

Samir Nasri (amezaliwa 26 Juni 1987) ni mchezaji wa kandanda wa kimataifa wa Ufaransa ambaye anaichezea klabu ya Arsenal katika ligi kuu ya Uingereza.

Samir Nasri mnamo mwaka 2012
Samir Nasri
Youth career
1993–2000Pennes Mirabeau
2000–2004Marseille
Senior career*
MiakaTimuApps(Gls)
2004–2008Marseille121(11)
2008–Arsenal34(6)
Timu ya Taifa ya Kandanda
2002–2003France U1618(8)
2003–2004France U1718(8)
2004–2005France U184(0)
2005–2006France U1910(5)
2006–2007France U214(0)
2007–Ufaransa15(2)
* Senior club appearances and goals counted for the domestic league only and correct as of 18:14, 13 Desemba 2009 (UTC).

† Appearances (Goals).

‡ National team caps and goals correct as of 18:14, 13 Desemba 2009 (UTC)

Yeye hutumia mguu wa kulia sanasana kucheza, na kwa ujumla hucheza kama mshambulizi mpana katika klabu yake ya Arsenal, lakini pia ametumika katika kiungo kati kwa majukumu ya kushambulia na kulinda wakati amehitajika. Amesifiwa na wengi kama " zizou mpya " (yaani mchezaji matata wa kitambo wa ufaransa, Zinedine Zidane) baada ya kufurahisha katika klabu ya Marseille wakati wa ujana wake.

Hapo awali alikuwa mchezaji wa kawaida wa timu ya Ufaransa katika kiwango cha vijana. Nasri alitajwa katika kikosi cha Euro mwaka wa 2008 lakini hakupata muda mwingi wa kucheza. Tangu wakati huo, amejiimarisha kama mchezaji wa kawaida katika timu ya taifa.

Maisha Yake ya Utotoni hariri

Wazazi wa Nasri walihamia Ufaransa kutoka Algeria. Babake anatoka Constantine na mama yake ni raia wa Biskra. Alilelewa katika sehemu ya La Gavotte Peyret,kitongoji kilicho kaskazini mwa Marseille. Mara nyingi yeye alicheza mitaani, ambapo alijifunza ujuzi wake. Alikuwa anaichezea timu ya genge ya mtaa, lakini baada ya vurugu nyingi, wazazi wake walimsaini katika klabu ya Pennes Mirabeau akiwa na umri wa miaka sita. Nasri mwenyewe amedai kuwa malezi yake ngumu imemsaidia katika jitihada zake za kucheza kandanda ya Utaalamu, "kama ninaweza kuwa na ujasiri wa kutosha wa kuonana ana kwa ana na kisu, nina ujasiri wa kutosha nina ujasiri wa kutosha kupambana mkabiliano mgumu. Aliichezea timu ya Pennes kwa muda wa misimu miwili kabla ya kutazamwa na Olympique de Marseille mwaka wa 1996.

Wasifu wa Klabu hariri

Marseille hariri

Nasri alianza kuicheza Marseille akiwa na umri wa miaka 9. Alianza kucheza katika Ligue 1 (ligi kuu ya Ufaransa) katika msimu wa 2004/2005 akiwa na umri wa miaka 17, na alianza mechi 13 na akaja kama mbadala mechi 11, na kufunga bao moja. Msimu uliyofuata ulimpa uzoefu katika kombe la UEFA (mechi 10 bila kufunga bao) na kombe la Intertoto (alicheza mechi moja na kufunga bao moja). Katika msimu wa 2006/2007 alifunga bao lake la kwanza la mwaka katika Ligue 1 msimu ukielekea kuisha tarehe 29 Aprili 2007, wakati alianza mechi dhidi ya FC Sochaux-Montbéliard na alisaidia timu yake kushinda 4-2. Ushindi huu uliifanya Marseille kupanda hadi nafasi ya nne katika Ligi 1 mechi nne zikisalia, na hivyo basi kuiweka Mairseille katika nafasi ya kufuzu katika Kombe la UEFA. Nasri alikuwa katika kikosi kilichoshindwa katika fainali ya Coupe de France mwaka 2006 dhidi ya Paris Saint-Germain na pia alikuwa katika kikosi kilichoshindwa katika fainali dhidi Sochaux mwaka wa 2007.

Tarehe 20 Mei 2007, Nasri alitajwa kama mchezaji mchanga bora wa mwaka katika Ligue 1 mbele ya Jimmy Briand na Karim Benzema. Alitajwa pia kama mchezaji bora wa mwaka wa Marseille baada ya kupata asilimia 62 ya kura kutoka kwa mashabiki. Aidha, kama wachezaji wachanga wengine, alitajwa kama " zizou mpya " kutokana na ujuzi wake wa kuchenga na mtazamo.

Arsenal hariri

 
Nasri inachukua corner kick kwa Arsenal

Nasri alifunga bao lake la kwanza katika Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya West Bromwich Albion, baada ya dakika nne ya mechi ya kwanza ya msimu, tarehe 16 Agosti 2008. Tarehe 27 Agosti katika mechi ya pili ya raundi ya kufuzu katika kombe la mabingwa barani Ulaya, Nasri alifunga bao katika dakika ya 26 dhidi ta FC Twente. Tarehe 8 Novemba 2008, Nasri alifunga mabao yote mawili ya Arsenal' katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Manchester United. Tarehe 21 Machi, Nasri alifunga bao tena Arsenal ilipoishinda Newcastle 3-1 katika uwanja wa St James 'Park. Alitamatisha msimu wake wa kwanza na Arsenal na mabao 7 na usaidizi 5.

Wasifu wa Kimataifa hariri

Nasri amekuwa akihusika katika timu ya taifa ya Ufaransa kwa muda mrefu, kuanzia timu za vijana wenye umri wa miaka 16, 17, 18, 19 na 21. Alikuwa katika timu ambayo ilishinda mashindano ya UEFA ya vijana wasiozidi umri wa 17 mwaka wa 2004, na alifunga bao la ushindi katika mechi ya mwisho. Nasri alicheza mechi yake ya kwanza ya timu kuu mnamo 28 Machi 2007 dhidi ya Austria, katika mechi ya kirafiki ya nyumbani akiwa na umri wa miaka 19. Alitoa pasi ndani ya boksi ambayo mchezaji mwenzake, Karim Benzema,alifunga bao la kipekee la mechi. Alifunga bao lake la kwanza katika mechi yake ya tatu katika timu kuu na Ufaransa ilishinda mechi hiyo, ambayo pia ilikuwa mechi ya kufuzu kushiriki katika kombe la Euro 2008,1-0 dhidi ya Georgia tarehe 6 Juni 2007. Nasri alitajwa katika kikosi cha mwisho cha Euro 2008 cha Raymond Domenech akiwa na umri wa miaka 20; alikuwa mmoja wa wachezaji wenye umri mdogo katika kikosi cha Kifaransa kuteuliwa katika mashindano ya Euro 2008. Alicheza mechi mbili kama mbadala na kucheza dakika 32.

Mbinu ya kucheza hariri

Nasri amelinganishwa na mchezaji wa kitambo wa Arsenal, Robert Pires, na Arsène Wenger ambaye pia amemweleza Nasri kama mchezaji mwenya kasi na mchezaji maalam anayeweza kucheza katika sehemu tofauti uwanjani na pia kuwaona wachezaji wenzake uwanjani.[1][1][1][1]

Maisha ya Kibinafsi. hariri

Samir amekuwa katika uhusiano na Tatiana Golovin ,mchezaji wa tenisi kutoka Ufaransa, tangu Mei 2008 na anaishi naye katika Hampstead.

Tuzo hariri

Marseille hariri

  • Kombe la UEFA la Intertoto: 2005

Kimataifa hariri

  • Mashindano ya kandanda ya bara Ulaya ya UEFA ya vijana wasiozidi umri wa miaka 17 ya mwaka wa 2004.

Kibinafsi hariri

  • mchezaji mchanga wa mwaka wa Ligue 1 : 2006-07
  • Timu ya Mwaka ya Ligue 1 : 2006-07

Takwimu za wasifu wa klabu hariri

(sahihi tangu 5 Desemba 2009)
Klabu Msimu Ligi Kombe [2][3] Ulaya Jumla
Matokeo Mabao Usaidizi Matokeo Mabao Usaidizi Matokeo Mabao Usaidizi Matokeo Mabao Usaidizi
Marseille 2004-05 24 1 -- 1 0 -- 0 0 0 25 1 --
2005-06 30 1 -- 5 0 -- 10 0 -- 45 1 --
2006-07 37 3 -- 7 0 -- 4 0 -- 48 3 --
2007-08 30 6 -- 4 0 -- 8 0 -- 42 6 --
Jumla [121] 11 -- 17 0 -- 22 0 -- 160 11 --
Arsenal 2008-09 29 6 2 5 0 3 10 1 0 44 7 5
2009-10 4 0 0 1 0 1 2 2 0 7 2 1
Jumla [33] 6 2 6 0 4 12 3 0 51 9 6
Jumla wa wasifu 154 17 2 23 0 4 34 3 0 211 20 6

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri