Samoa ya Marekani (kwa Kisamoa: Amerika Samoa au Samoa Amelika) ni Eneo la ng'ambo la Marekani katika bahari ya Pasifiki upande wa kusini wa nchi huru ya Samoa.

Bank Kuu Ya Samoa
Samoa ya Marekani

Kuna wakazi 54,719 (wengi wakiwa wametokana na wakazi asili) katika eneo la nchi kavu la km² 199.

Eneo lake ni sehemu ya funguvisiwa la Samoa. Kutokea kwa eneo la pekee kulisababishwa na ukoloni wa karne ya 19 ambako Ujerumani na Marekani zilishindana juu ya visiwa hivyo. Funguvisiwa liligawiwa kwa mkataba wa Berlin wa 1899. Sehemu ya mashariki ikawa upande wa Marekani na sehemu ya magharibi upande wa Ujerumani.

Kwa katiba ya mwaka 1967 Samoa ya Marekani ilipewa madaraka ya kujitawala.

Upande wa dini, karibu wote ni Wakristo, hasa Wakalvini (50%) na Wakatoliki (20%), kama si Wamormoni.

Tazama pia hariri


  Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.