Saruji ya Bamburi ni mojawapo ya makampuni kubwa zaidi ya kutengeneza saruji katika eneo la barani Afrika lililoko chini ya jangwa la Sahara. Kampuni hii imeorodheshwa katika Soko la Hisa la Nairobi na jina lake kwa ufupi ni BCC (Bamburi Cement Company).

Nembo ya Saruji ya Bamburi

Saruji ya Bamburi iko na shughuli katika eneo la Bamburi katika maeneo ya mashambani ya Mombasa na Nairobi. Kituo chao kikuu kiko katika jiji Nairobi.

Historia hariri

Saruji ya Bamburi ilianzishwa mwaka 1951 na Felix Mandi, aliyekuwa mkurugenzi katika kampuni ya saruji ya Cementia Holding A.G. Zurich. Baadaye, Cementia iliunda muungano na kampuni ya Blue Circle PLC (UK). Mwaka 1989, kampuni ya Lafarge, kampuni kubwa zaidi duniani ya vyombo vya kujengea, ilinunua Clement, na kwa hivyo, ikawa na hisa sawa na Blue Circle PLC. Lafarge ilinunua Blue Circle mwaka 2001 na hili liliifanya iwe kampuni kubwa zaidi ya vyombo vya ujenzi na Saruji ya Bamburi kama mshikilia hisa mkuu.

Kiwanda chao cha kwanza cha Mombasa kilianza kutoa Saruji mwaka 1954, kikiwa na uwezo wa mwaka wa toni 140,000 ya saruji. Leo, kiwanda hiki kina uwezo wa kutoa toni milioni 1.1 ya saruji kwa mwaka.

Mwaka 1998, kiwanda kilichokuwa na uwezo wa toni milioni 2.1 kwa mwaka cha kusagia simiti kilijengwa nje tu ya Nairobi. Kiwanda hiki kiliongeza uwezo wa kampuni hii hadi toni milioni 2.1. Kwa sababu ya kiwanda hiki, Saruji ya Bamburi sasa inaweza kuimarisha utenda-kazi wake kwa wakazi wa Nairobi na Soko za mashambani. Reli inayopitia kiwanda hiki pia kimesaidia mauzo katika maeneo ya Magharibi ya Kenya na Uganda.

Saruji ya Bamburi pia ni mojawapo ya makampuni yanayoleta pesa mingi zaidi kutoka nje nchini Kenya, kwa kusafirisha asilimia 28 ya saruji yake nje mwaka 1998. Soko za nje ni kama Reunion, Uganda na Mayotie. Kitambo, walikuwa wakiuzia Mauritius, Sri Lanka, Comoros, Madagascar, Seychelles na Congo.

Marejeo hariri

Viungo vya Nje hariri