Sila au Siluano (kwa Kigiriki: Σίλας / Σιλουανός; karne ya 1 AD) ni mmojawapo kati ya viongozi muhimu zaidi wa Kanisa la mwanzo huko Yerusalemu[1].

Mt. Sila.

Kutoka huko alitumwa mara nyingi kwa Wakristo wasio Wayahudi kushughulikia matatizo mbalimbali (kuanzia Mdo 15:22) akawa mwenzi wa Mtume Paulo katika safari za kimisionari (kuanzia Mdo 16:25) akatimiza hadi mwisho huduma zake kwa neema ya Mungu na bidii isiyokubali kuchoka.

Anatajwa na Paulo katika barua mbalimbali (k.mf. 2Kor 1:19).

Hatimaye alimsaidia Mtume Petro kuandika waraka yake wa kwanza (1 Pet 5:12).[2]

Anaheshimiwa na madhehebu mengi ya Ukristo kama mtakatifu, ila tarehe ya sikukuu yake ni tofautofauti. Kwa Wakatoliki ni tarehe 13 Julai[3].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. https://www.santiebeati.it/dettaglio/90225
  2. "Notes on 1 Peter". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-10-03. Iliwekwa mnamo 2012-08-14. 
  3. Martyrologium Romanum
  Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sila kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.