Stafeli (kutoka jina la Kihindi; kwa Kiingereza soursop) ni tunda la mstafeli (Annona muricata) lenye rangi ya kijani nje, nyama nyeupe, laini na tamu na mbegu nyeusi.

Stafeli mtini.
Stafeli lililoiva.

Matumizi hariri

Majani hutumika kama chai ili kutibu mafua na kuhara damu, na pia husaidia mfumo wa umeng'enyaji wa chakula.

Mizizi ya mstafeli huua minyoo wa aina mbalimbali, wakati kutoka mbegu zake hutengenezwa dawa za kufukuza wadudu waharibifu n.k.

Inadaiwa kwamba stafeli au juisi yake huponya saratani au hupunguza ukali wa dawa za saratani. Lakini uchunguzi wa kisayansi haukuweza kuhakikisha hii[1][2][3].

Marejeo hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Stafeli kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.