Steven Kanumba

Muigizaji wa filamu, mwandishi na mkurugenzi (1984-2012)

Steven Charles Kanumba (alizaliwa mnamo tarehe 8 Januari 1984,[1]katika mkoa wa Shinyanga - alifariki tarehe 7 Aprili 2012 [2]) alikuwa msanii wa maigizo na filamu kutoka nchini Tanzania,baba yake alikuwa anaitwa Charles Kanumba na mama yake aliitwa Flora Mutegoa.Alikuwa ana uwezo wa kuongea lugha 3: kiswahili, kisukuma na kiingereza. Ni mmoja wa wasanii wa kwanza kufanya kazi nje ya Nchi na kuvutia wasanii wa nje kuja kuigiza nchini Tanzania. Hasa walikuwa Wanigeria kama vile Mercy Johnson, Emmanuel France, Nkiru Silvanus , Ramsey Nouah [3] na wengineo. Kanumba pia ameweza kuwaleta waongozaji filamu kadhaa wa Kinigeria nchini.

Steven Kanumba

Hayati Steven Kanumba.
Amezaliwa Steven Charles Kanumba
Januari 8 1984 (1984-01-08) (umri 40) Shinyanga, Tanzania
Amekufa Aprili 7, 2012 (umri 28) Dar es Salaam, Tanzania
Kazi yake Muigizaji, Mtunzi, Mtayarishaji, Muongozaji

Maisha

Steven Alianza elimu yake ya msingi katika shule ya Shule ya msingi Bugoyi na aliendelea na elimu ya sekondari katika shule iliyoitwa Shule ya sekondari Mwadui, Na baadae aliamishiwa Vosa Mission Secondary School . Alijiunga kidato cha 5 & 6 katika Shule ya Sekondari Jitegemee[4] iliyopo Dar-es-salaam

Shughuli za uigizaji

Kanumba ameanza shughuli za kuigiza miaka mingi kwenye miaka ya 1990. Ambapo alianza kufahamika zaidi mwaka 2002 mara tu baada ya kujiunga na kundi la sanaa ya maigizo maarufu kama Kaole Sanaa Group lililopo Bagamoyo. Alijibebea umaarufu mkubwa nchini Tanzania na alikuwa kipenzi cha wengi na alikubalika karibia nchi zote za Afrika Mashariki na maziwa makuu. Aliweza kutangaza sanaa nchi za Afrika ya Magharibi ikiwemo Nigeria na pia Wanigeria walipendezewa na uigizaji wake hivyo kushirikiana pamoja naye katika filamu kadha wa kadha. Filamu ambazo aliwahi kuigiza ni Dar to Lagospamoja na She is My Sister .

Kifo

Kanumba alifariki baada ya kupata jeraha kwenye ubungo, ambapo jeraha hilo lilisabishwa baada ya kupata pigo kichwani tarehe 07/04/ 2012 [5] ILisemekana alikuwa na rafiki yake wa kike anayeitwa Elizabeth Michael anaye fahamika kama Lulu ambaye alikuwa na miaka 18 kipindi hicho. Lakini rafiki yake huyo alikanusha kuhusu kuhusika na kifo cha Kanumba.[6] Kanumba alipelekwa hospitali ya taifa Muhimbili akiwa mahututi ambapo, baada ya vipimo madktari walithibitisha kwamba kifo chake kilitokana na jeraha kwenye ubungo kumsababishia kukosa pumzi na kupoteza uhai hapo. Mnamo mwaka 2017, Lulu alituhumiwa kwa kuua bila kukusudia na alipewa adhabu ya kufungwa miaka 2.[7] Hukumu yake ilibadilishwa na kufanya huduma za kijamii aliachiwa jela baada ya kifungo cha mwaka mmoja released from jail 12/05 /2018. Msiba wake ulihudhuriwa na watu takribani 30,000 akiwepo mheshimiwa mama Salma Kikwete. Alizikwa katika makaburi ya Kinondoni.

Filmografia

Televisheni

  • Jahazi
  • Dira
  • Zizimo
  • Tufani
  • Sayari
  • Taswira
  • Gharika
  • Baragumu

Filamu

Mwaka Jina Maelezo
Haviliki
Neno
Ulingo
Riziki akiwa na Blandina Chagula
Sikitiko Langu akiwa na Nuru Nassoro, Vincent Kigosi, Ally Chaowa na Mahsein Awadh
Dangerous Desire akiwa na Vincent Kigosi, Nuru Nasoro and Blandina Chagula
She is My Sister akiwa na Mercy Johnson, Nkiru Sylvanus na Yvonne Cherryl
Penina akiwa na Mahsein Awadh, Emmanuel Myamba
Cross My Sin akiwa na Mercy Johnson, Suzan Lewis
2007 A Point Of No Return akiwa na Wema Sepetu, Mahsein Awadh
2008 The Lost Twins akiwa na Lucky Peter, Elizabeth Michael, Suzan Lewis
The Stolen Will akiwa na Eizabeth Chijumba, Immaculate Aloyce
Village Pastor akiwa na Aunt Ezekiel
Magic House akiwa na Nargis Mohamed, Issa Mussa
Oprah akiwa na Irene Uwoya na Vincent Kigosi
Red Valentine akiwa na Wema Sepetu, Jacquline Wolper
*Family Tears akiwa na Elizabeth Michael, Wema Sepetu na Richard Bezednhout
The Movie's Director akiwa na Mercy Johnson, Nkiru Sylvanus, Elizabeth Chijumba, Olufemi Ogdegbe
Fake Smile akiwa na Aunt Ezekiel, Yobnesh Yusuph
Unfortunate Love akiwa na Lisa Jensen, Aunt Ezekiel, Elizabeth Michael
Hero Of The Church akiwa na Princess Sheila, Issa Musa, Juma Kilowoko
Saturday Morning akiwa na Shamsa Ford, Hemed Suleiman, Issa Musa
Shauku
Crazy Love akiwa na Shamsa Ford, Hemed Suleiman, Issa Musa, Elizabeth Michael
2006 Johari[8] akiwa na Blandina Chagula na Vincent Kigosi)
2006 Dar 2 Lagos[8] akiwa na Mercy Johnson, Nancy Okeke, Bimbo Akintola
2010 More Than Pain akiwa na Lisa Jensen na Rose Ndauka
2010 Young Billionare akiwa na Aunty Ezekiel na Patcho Mwamba
2010 "Ripple of Tears" akiwa na Elizabeth Michael
2010 Uncle JJ
2010 This Is It
2010 Off Side akiwa na Irene Uwoya, Vincent Kigosi NA Jacob Steven
2010 Payback akiwa na Yvonne Cherryl, Yusuph Mlela
2010 Black Sunday akiwa na Yvonne Cherryl, Yusuph Mlela, Hemed Suleiman)
2010 Young Billionare akiwa na Aunty Ezekiel and Patcho Mwamba
2011 Saturday Morning akiwa na Irene Paul na Ben Franko
2011 Deception akiwa na Rose Ndauka, Patcho Mwamba, Bakari Makuka
2011 Devil Kingdom akiwa na Ramsey Noah, Kajala Masanja
2011 The Shock akiwa na Shazy Sadry
2011 Moses (filamu)Moses akiwa na Suzan Lewis, Shazy Sadri, Ndumbangwe Misayo
2012 Big Daddy
2012 Because of You akiwa na Rose Ndauka na Grace Mapunda
2012 Ndoa Yangu akiwa na Jacquline Wolper na Patcho Mwamba
2013 Love & Power akiwa na Irene Paul na Patcho Mwamba; filamu ya mwisho ya Kanumba

Marejeo

  Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Steven Kanumba kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.