Tatata
Tatata mbavu-nyeupe (Batis molitor)
Tatata mbavu-nyeupe (Batis molitor)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Corvoidea (Ndege kama kunguru)
Familia: Platysteiridae (Ndege walio na mnasaba na bwiru)
Jenasi: Batis
Boie, 1833
Ngazi za chini

Spishi 20:

Tatata au kapurapunda ni ndege wadogo wa jenasi Batis katika familia Platysteiridae wanaotokea Afrika chini ya Sahara. Zamani waliainishwa katika familia Muscicapidae. Takriban spishi zote zina kinyago cheusi, utosi kijivu, mgongo kijivu au mweusi, tumbo jeupe na kidari chenye mlia mweusi au kahawiachekundu. Dume ana nyeusi zaidi na jike ana nyekundu zaidi. Hula wadudu na hulijenga tago lao kwa umbo wa kikombe katika mti au kichaka. Jike huyataga mayai 1-4.

Spishi hariri

Picha hariri