Timone mwinjilisti

Timone mwinjilisti ni Myahudi wa karne ya 1 anayejulikana hasa kutokana na Matendo ya Mitume.

Mchoro wa ukutani wa Fra Angelico, ukionyesha Mtume Petro akiweka wakfu wainjilisti saba wa kwanza.

Anaheshimiwa na madhehebu mbalimbali ya Ukristo kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa na Kanisa Katoliki na Anglikana tarehe 28 Julai pamoja na wenzake Prokoro, Nikanori, Parmena na Nikola wa Antiokia[1][2].

Katika Biblia hariri

Alikuwa mmojawapo kati ya wanaume saba wa lugha ya Kigiriki katika Kanisa mama la Yerusalemu ambao, wakiwa wamejaa Roho Mtakatifu na hekima, walichaguliwa na waumini wenzao wakawekewa mikono na Mitume wa Yesu ili kushughulikia kwa niaba yao huduma za fukara (Mdo 6)[3].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. "Martyrologium Romanum", Typis Vaticanis, Editio Altera, 2004
  2. Calendar of saints (Episcopal Church in the United States of America)
  3. https://www.santiebeati.it/dettaglio/91953