Tufe ni umbo la gimba linalofanana na mpira au chungwa. Lakini wala mpira wala chungwa ni tufe kamili.

Picha ya tufe
Rediasi au nusukipenyo (= r) cha tufe

Katika elimu ya hisabati, hasa jiometri tufe ni jumla la nukta zote zilizopo na umbali uleule (=rediasi, nusukipenyo) kutoka nukta nukta moja (kitovu cha tufe).

Tufe ni mzunguko wa duara katika wanda (dimension) la tatu.

  • Kitovu cha tufe ni nukta iliyopo katikati yake yenye umbali sawa na kila nukta kwenye uso wake.
  • Nusukipenyo cha tufe ni umbali kati ya kitovu chake hadi nukta yoyote kwenye uso wake
  • Uso wa tufe ni eneo linalojumlisha nukta zote zenye umbali wa nusukipenyo kutoka kitovu


Mjao hariri

Mjao wa tufe (=V) unaelezwa kwa fomula ifuatayo:

 

  (tamka pi) ni namba ya duara inayolingana takriban na 3.1416.

Eneo la uso wa tufe hariri

Eneo la uso wa tufe (=A) hukadiriwa kufuatana na fomula ifuatayo:

 

Viungo vya Nje hariri