Uchaguzi wa Rais wa Marekani, 1856

Uchaguzi wa 1856

Uchaguzi wa Rais wa Marekani, mwaka wa 1856 ulikuwa wa 18 katika historia ya Marekani. Ukafanywa Jumanne tarehe 4 Novemba. Upande wa "Democratic Party", James Buchanan (pamoja na kaimu wake John Breckinridge) aliwashinda mgombea wa "Republican Party" John Frémont (pamoja na kaimu wake William Dayton) na mgombea wa "Know-Nothing Party", Rais wa zamani Millard Fillmore (pamoja na kaimu wake Andrew Donelson).

Matokeo hariri

Buchanan akapata kura 174, Frémont 114 na Fillmore nane tu. Ramani yaonyesha kura kwa kila jimbo.