Uchaguzi wa Rais wa Marekani, 1952

Uchaguzi wa Rais wa Marekani, mwaka wa 1952 ulikuwa wa 42 katika historia ya Marekani. Ukafanywa Jumanne tarehe 4 Novemba. Upande wa "Republican Party", Dwight Eisenhower (pamoja na kaimu wake Richard Nixon) alimshinda mgombea wa "Democratic Party" Adlai Stevenson II (pamoja na kaimu wake John Sparkman).

Matokeo hariri

Eisenhower akapata kura 442, na Stevenson 89. Ramani yaonyesha kura kwa kila jimbo.