Uchaguzi wa Rais wa Marekani, 1988

Uchaguzi wa Rais wa Marekani, mwaka wa 1988 ulikuwa wa 51 katika historia ya Marekani. Ukafanywa Jumanne tarehe 8 Novemba. Upande wa "Republican Party", mgombea George H. Bush (pamoja na kaimu wake Dan Quayle) alimshinda mgombea wa "Democratic Party" Michael Dukakis (pamoja na kaimu wake Lloyd Bentsen).

Matokeo hariri

Bush akapata kura 426, na Dukakis 111 wakati mchaguzi mmoja kutoka West Virginia alimpigia kura Bentsen badala ya Dukakis. Ramani yaonyesha kura kwa kila jimbo.