Waeseni walikuwa madhehebu mojawapo ya Uyahudi katika karne ya 1 KK na karne ya 1 B.K. Walikoma wakati wa vita vya ukombozi dhidi ya wakoloni wa Dola la Roma. Biblia haiwataji kamwe, lakini wanajulikana kupitia vitabu vingine, hasa vile vilivyopatikana katika pango la Qumran, lililohifadhi kwa miaka karibu 1900 maktaba ya jumuia yao iliyokuwa inaishi huko katika mazingira ya jangwa ili kujiandaa kupokea ufalme wa Mungu. Msimamo wao ulikuwa mkali kabisa, ndiyo sababu wengi wao walijitenga na Wayahudi wenzao pia. Labda ndio waliomlea mtoto Yohane Mbatizaji.

Mahali yalipopatikana magombo ya Waeseni, karibu na korongo la Qumran

Viungo vya nje hariri