Wilhelm Caspar Oddo

Wilhelm Caspar Oddo ( alizaliwa mkoani Mbeya, Aprili 2 1987 (1987-04-02) (umri 37) ni Mwana Tehama, Mwandishi, Mjasiriamali Jamii na Mfanyabiashara. Anafahamika zaidi kwa kuwa muasisi wa Chuo cha NLab Innovation Academy ambacho kabla ya kuwa chuo ilikuwa na Hatamizi ya wazi kwa wanafunzi na vijana ili kuweza jifunza kutengeneza mifumo ya kitehama bure pasipo malipo yoyote huku ikiwasaidia vijana wakike na wakiume kuanzisha miradi yenye kusaidia jamii na kutengeneza mazingira mazuri ya wao kuweza pata nafasi za masomo ya juu na fursa mbali mbali[1]. Pia ni muasisi mwenza wa Taasisi za NLab Foundation na Apps and Girls.

Maisha ya awali na elimu hariri

Alizaliwa mkoani mbeya na kukulia mkoani Njombe akiwa ni mtoto wa Pili kati ya watatu. Shule ya awali alisoma shule kadhaa ikiwemo Kililo Primary School - Mbeya, Lugarawa Primary School - Njombe na Mtera Dam Primary school - Dodoma. Secondary alisoma Mtera Secondary School (Ladwa) na baadaye kujiunga na Kidato cha tano na sita katika shule ya Secondary ya Biafra iliyo kuwepo Kinondoni Jijini Dar es salaam. Akiwa kidato cha Sita alipata ajali mbaya ya gari iliyobadilisha maisha yake kwa ujumla.

Alijiunga na Chuo kikuu cha Kampala International University mwaka 2007 na kuhitimu mwaka 2010 ambako alipata shahada ya sayansi ya mifumo ya taarifa (Information System).

Kazi hariri

Mwaka 2010 mwishoni aliajiriwa kama Mkufunzi msaidizi huku akisoma Shahada ya utengenezaji wa Mifumo ya Compyuta (Masters of Science in Software Engineering). Mwaka 2014 mwishoni aliacha kazi rasmi na kuanzisha Hatamizi ya wazi iliyo itwa OUFLab huko Gongo la mboto jijini Dar es salaam.

Kazi za Kijamii hariri

  1. OUFLab : Mwaka 2010 mara baada ya kumaliza chuo na kuajiriwa kama Mkufunzi msaidizi katika chuo kikuu cha Kampala International University tawi la Dar Es Salaam, Wilhelm aliona tatizo kwa wanafunzi aliokuwa akiwafundisha. Wengi walitamani kuwa watengenezaji wazuri wa Mifumo na tovuti lakini changamoto ilikuwa ni ugumu wa Masomo hayo ya Kutengeneza mifumo na zaidi elimu yao ya nyuma haikuwa na msingi mzuri wenye kumfanya mwanafunzi aweze kuielewa vyema lugha ya uandishi wa Codes zenye kutengeneza mifumo hiyo. Wilhelm akaanzisha utaratibu wa kuwafundisha wanafunzi kutoka vyuo mbali mbali nyumbani kwake Mzambarauni Gongo la Mboto. Na mradi huu ulioitwa OUFLab[2] ukawa ni mradi maarufu na wenye kuvutia wanafunzi kutoka vyuo mbali mbali kama UDSM, IFM, KIU na vinginevyo.
  2. Friday Night Code: Huu ulikuwa ni mradi wa kuwakutanisha wanafunzi wa vyu mbali mbali siku ya Ijumaa jioni, wanafunzi walikuwa wakikutana Nyumbani kwa Wilhelm na kuanza kusaidiana kutengeneza mifumo usiku mzima na ifikapo asubuhi ya saa Moja wote hutawanyika na kuendelea na shughuri zao nyingine. Mmoja wa wawezeshaji katika Friday Night Code alikuwa ni Carolyne Ekyarisiima ambaye naye alikuwa ni Mkufunzi katika chuo kikuu cha Kampala International University tawi la Dar es salaam[3].
  3. Mafunzo ya TEHAMA kwa watoto: Hakuishia hapo, Wilhelm akaona kuna haja ya kurudi nyuma na kuanza waandaa hawa ambao wangetamani kuwa Waundaji wa mifumo ya Kitehama, na kwakuwa mtaala wa elimu ya msingi haukuwa na mafunzo hayo hivyo mwaka 2013 akaanzisha mafunzo kwa watoto, nayo yakifanyikia nyumbani kwake huko huko Gongo la Mboto.[4]
  4. Walimu na Tehama: Katika kuchangia juhudi za kuboresha elimu ya Tanzania Wilhelm na timu yake wakaanzisha mradi wa kufundisha Tehama kwa walimu. Mradi ulianzia NLab na baadaye kuanza zunguka mashuleni kufundisha Tehama. mafunzo yalihusisha utengenezaji wa tovuti kwa kutumia mifumo wazi ya Wordpress na Joomla, pia matumizi ya TEHAMA katika kuandaa nyenzo na matirio ya kufundishia wawapo darasani. Pia walimu wakafundishwa namna sahihi ya kutunza taarifa zao wawapo mtandaoni.

Biashara hariri

Wilhelm amejikita kwenye biashara zinazo husu elimu, fedha, kilimo na ufugaji.

Mijadala , Mihadhara na Mazungumzo hariri

Amekuwa ni mshiriki katika Mihadhara ndani na nje ya Tanzania inayo husisha elimu, kilimo, vijana, ajira, afya, mazingira na Ujinsia.

  1. Mkutano wa E-Learning Africa (Rwanda) mwaka 2018 - Alizungumzia (Changing the Future of Africa, One Step at a Time)[5]

Vitabu alivyo andika hariri

  1. Hatua kwa Hatua: ISBN: 978 9987 9642 1 5
  2. Lawama: ISBN: 978 9987 9642 1 5
  3. Insights: A Youth's Guide to Business Success: ISBN: 978 9987 9642 2 2

Tuzo na Teuzi hariri

  1. Private Sector Youth Inclusive Award - Ghana (2020)[6]
  2. AvanceMedia Most Influential Young Tanzanians (2018)[7]

Marejeo hariri

  1. https://se-forum.se/interviews/fighting-poverty-youth-unemployment-ict-education/
  2. https://www.thecitizen.co.tz/tanzania/magazines/sound-living/bridging-the-digital-divide-2630106
  3. "Friday Night Code: Where Passion Meets Progress". East Africa Pulse. Iliwekwa mnamo 2024-04-11. 
  4. https://www.thecitizen.co.tz/tanzania/magazines/success/africa-s-education-efforts-are-shifting-in-order-to-reflect-ict-growth-2513576
  5. https://www.elearning-africa.com/programme/pdf/eLA2018_programme.pdf
  6. "Private Sector Youth Inclusive Award". Youth SDG Achievers Awards (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2024-04-11. 
  7. "Celebrating Tanzania’s Most Influential Young Entrepreneurs". East Africa Pulse. Iliwekwa mnamo 2024-04-11. 

Viungo vya nje hariri

  1. https://www.bz-berlin.de/archiv-artikel/b-z-reporterin-suchte-eine-app-in-afrika
  2. https://www.oneyoungworld.com/blog/young-leaders-bringing-smile-unhappiest-countries-earth
  3. https://eastafricapulse.blogspot.com/2018/11/education-institution-from-tanzania.html
  4. http://tz.avancemedia.org/
  5. https://www.indiegogo.com/projects/community-owned-computer-lab-in-tanzania#/
  6. https://medium.com/startupbus/buspreneur-interview-with-wilhelm-oddo-793f02961936
  7. https://tanzict.wordpress.com/2013/10/01/pitching-session-for-startups-congratulations-to-victronix/
  8. https://www.torial.com/anne-lena.moesken/contents/245490
  9. https://www.ghanaweb.com/GhanaHomePage/africa/Kuami-Eugene-Kwadwo-Sheldon-JoeBoy-among-129-young-Africans-nominated-for-2020-Africa-Youth-Awards-1134104#google_vignette
  10. https://pulte.nd.edu/news/notre-dame-president-rev-john-i-jenkins-c-s-c-welcomes-2018-mandela-washington-fellows-to-campus/
  11. https://www.modernghana.com/entertainment/65403/kuami-eugene-kwadwo-sheldon-joeboy-among-129.html
  12. https://www.oneyoungworld.com/news-item/calloncop-advocating-action-climate-change
  13. https://www.yalieastafrica.org/faq/images/The%20Leading%20Edge%20Issue%205.pdf
  14. https://eastafricapulse.blogspot.com/2021/03/empowering-next-generation-of-tech.html
  15. https://sdgachieversawards.org/speaker/private-sector-youth-inclusive-award/