Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (Kiingereza: Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation kifupi (MFAIC)) ni wizara ya serikali nchini Tanzania. Ofisi kuu ya wizara hii zipo mjini Dar es Salaam.

Jinsi ilivyo kwa wizara ya mambo ya nje, kazi yake ni kuwakilisha Tanzania kimataifa, kuwasiliana na serikali za nje na taasisi za kimataifa kama Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika na taasisi zake, kuendesha balozi za Tanzania katika nchi nyingine na kutoa visa kwa wageni wanaotaka kuja Tanzania, na kushirikiana na wizara nyingine za Tanzania.

Marejeo hariri

Tazama pia hariri

Viungo vya nje hariri