Yakobo Mkatwakatwa

Yakobo Mkatwakatwa (alifariki Beth Lapat, nchini Uajemi, 421) alikuwa askari Mkristo aliyeuawa kwa sababu ya imani yake katika dhuluma ya mfalme Yazdegerd I[1]. Ingawa kwanza alikubali kuasi, alipolaumiwa na familia yake alitubu na hatimaye alivumilia kukatwakatwa sehemu 28 kabla ya kukatwa kichwa[2].

Mchoro mdogo wa kifodini cha Mt. Yakobo, katika Menologion of Basil II.

Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi, Waorthodoksi wa Mashariki na Wakatoliki kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 27 Novemba[3].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/91626
  2. John J. Delaney, Dictionary of saints, (Image, 2005), 323.
  3. Martyrologium Romanum

Marejeo hariri

  • Thieleman J. van Braght, Martyr's Mirror, 1660

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.