Zhongtong ni jina la kampuni inayotengeneza mabasi nchini China. Kiwanda kipo katika mji wa Liaocheng katika Jimbo la Shangdong. Kampuni imeorodheshwa katika soko la hisa la Shenzhen, na ni mmoja wa watengenezaji mabasi wakubwa wa China[1].

Basi la Zhongtong
Nembo ya Zhongtong

Historia

hariri

Kampuni hii ilianzishwa mwaka 1958. Liaocheng kama viwanda vya kutengeneza mabasi, walianza kutengeneza mabasi mwaka 1971. Baada ya mfululizo wa mabadiliko ya jina sasa ni mabasi ya Zhongtong, mwaka 1998.

Mwaka 2017 walikuwa na wafanyakazi 4,000 waliotengeneza kwenye eneo la m² 934,000.[2]


Marejeo

hariri
  1. http://english.mofcom.gov.cn/aarticle/newsrelease/commonnews/200703/20070304455301.html
  2. About Zhogdong, tovuti ya wenyewe, iliangaliwa Machi 2018