Kwa ziwa lenye jina la karibu angalia Assale (Ethiopia)

Ziwa Assal
Mahali Bonde la Afra
Anwani ya kijiografia 11°39′N 42°25′E / 11.650°N 42.417°E / 11.650; 42.417
Aina ya ziwa Ziwa la Crater
Mito ya kuingia chini ya ardhi kutoka bahari
Mito ya kutoka hakuna
beseni 900 km2
Nchi za beseni Jibuti
Urefu 10 km
Upana 7 km
Eneo la maji 54 km2
Kina cha wastani 7.4 m
Kina kikubwa > 20 m
Mjao 400 million m3
Kimo cha uso wa maji juu ya UB -155 m
Miji mikubwa ufukoni Randa 25 km Kaskazini-Mashariki)

Ziwa Assal (kwa Kifaransa Lac Assal) ni ziwa la chumvi lililopo nchini Jibuti. Liko katika mpaka wa kusini wa mkoa mwa Tadjoura, ikigusa eneo la mkoa wa Dikhil, takribani km 120 magharibi mwa Mji wa Jibuti.

Liko m 155 chini ya usawa wa bahari katika Bonde la Afar. Fuo zake zinashirikisha eneo la chini zaidi barani Afrika na ni ya pili ya chini zaidi duniani baada ya Bahari ya Chumvi huko Israeli/Palestina/Jordan.

Urefu wake mkubwa unafikia kilomita 19 na upana wake mkubwa hadi km 7; eneo la maji yake ni hadi km² 54. Kina cha juu kinafikia hadi mita 40. Beseni lake inajumlisha maeneo ya km² 900.

Ziwa hili halina njia ya kutoka kwa maji isipokuwa uvukizaji. Tokeo lake, ilhali maji ya kuingia yana kiasi cha chumvi ndani yake, ni kwamba kiwango cha chumvi katika maji ya ziwa kinazidi kuongezeka. Leo hii ni ziwa lenye chumvi nyingi duniani [1] kushinda Bahari ya Chumvi.

Eneo la ziwa hili ni kama jangwa na hakuna mimea wala wanyama waonekanao ila mimea midogo katikati ya ziwa hilo.

Kipimo cha juu cha halijoto katika eneo hilo hufanya maji kugeuka ukungu kwa urahisi, kwa hiyo eneo hilo limezungukwa na mwamba wa chumvi iliyoshikamana.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. isipokuwa maziwa machache kwenye bara la Antaktika yaliyopimwa kuwa na chumvi zaidi

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ziwa Assal kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.