Kiajemi

(Elekezwa kutoka زبان فارسی)

Kiajemi au Farsi (فارسی) ni lugha ya taifa ya Uajemi. Ni kati ya lugha za Kihindi-Kiajemi, ambazo tena ni kati ya lugha za Kihindi-Kiulaya. Inaandikwa kwa herufi za Kiarabu ambamo herufi nne za ziadi zimeongezwa kwa kutaja sauti zizizoweza kuonyeshwa kwa Kiarabu asilia. Hizi herufi za ziada ni پ p, چ ch, ژ zh na گ g.

Kiajemi ilikuwa na athira kubwa juu ya lugha mbalimbali hasa Kiarabu na Kituruki.

Inatumiwa hasa katika nchi zifuatazo:

Kuna wasemaji wa lugha ya kwanza milioni 70, na takriban wasemaji wengine milioni 60 kama lugha ya pili.

  • Katika Afghanistan yenye wasemaji takriban milioni 15 lugha inaitwa "dari" (درى).
  • Katika Tajikistani yenye wasemaji milioni 15 pia lugha inaitwa "Kitajiki".

Kutokana na uhamiaji wa karne ya 20 lugha inapatikana katika nchi nyingi za dunia. Persian Language Location Map.svg

Viungo vya njeEdit