AIESEC (hutamkwa "ai-seki", awali ni kifupi kwa Association Internationale des Sciences Étudiants sw Économiques et Commerciales ') ni shirika la kimataifa la vijana ambalo linajihusisha katika kubadilishana wanafunzi wa kimataifa na programu za tarajali kwa mashirika yafanyayo kazi kwa faida na yale yasiyo ya faida. Ofisi zake za kimataifa ziko Rotterdam, Uholanzi.

Mtandao wa AIESEC mnamo Juni 2009 ulijumuisha zaidi ya wanafunzi 38,000 katika nchi na maeneo 107. AIESEC ipo katika zaidi ya vyuo vikuu 1700 duniani kote, na hutuma wanafunzi kwenye programu 5500 za kubadilishana wanafunzi kwa mwaka[1]

Historia hariri

Wazo kuu kuhusu AIESEC lilianza katika miaka ya 1930, wakati wawakilishi kutoka shule za Ulaya walipokuwa wakibadilishana habari kuhusu mipango tofauti na shule maalumu katika biashara na uchumi. Wanafunzi walikuwa wakifanya tarajali katika nchi zingine, lakini hasa kwa juhudi zao wenyewe, na yote hii ikasimama baada kuanza kwa Vita ya Pili ya dunia[2] Mwaka 1944, ingawa nchi zilizokuwa hazifungamani na upande wowote za Skandinavia zilikuwa bado zinabadilishana wanafunzi: Stockholm, Bertil Hedberg (Ofisa katika Shule ya Uchumi ya Stockholm) na wanafunzi wawili Jaroslav Zich wa Chekoslovakia na Stanislas Callens wa Ubeligiji walianzisha "AIESE", iliyoitangulia AIESEC. [2]

Shughuli rasmi za "kusaidia kuendeleza 'mahusiano ya kirafiki' kati ya nchi wanachama" yalianza mwaka 1946, na AIESEC kwa mara ya kwanza ilianzishwa rasmi mwaka 1948. Wakati huo, misheni ilikuwa "kupanua uelewa wa taifa n kupanua uelewa wa watu binafsi, kubadilisha ulimwengu kwa mtu mmoja kwa wakati." [2] Mwaka 1949, wanafunzi 89 walishiriki katika iliyoitwa "Stockholm Congress ", iliyokuwa ya kwanza kati ya "Programu za Kubadilishana wanafunzi" nyingi. [3] Ndani ya mda mfupi, AIESEC ikawa maarufu: mnamo mwisho wa mwaka 1960, mabadilishano 2467 yaliripotiwa na mabadilishano 4232 ilipofika mwisho wa mwaka 1970. Hatua kubwa katika historia ya AIESEC ilikuja wakati "Dhima ya programu ya kimataifa" ilipoanzisha rasmi semina za kimataifa, kikanda, na mitaa kuhusu mada maalumu, ambayo baada ya mda ilikuwa na kuwa mwongozo wa AIESEC kwa vizazi vilivofuata baadaye. [3] Katika miongo iliyofuata, mada za majadiliano zilikuwa Biashara za Kimataifa, Elimu ya Manejimenti, maendeleo endelevu, Ujasiliamali na Majukumu ya Ushirika, [3] na katika miaka ya 1990, mtandao wa ndani ulioitwa Insight ulianzishwa kuwezesha mitandao. [3]

AIESEC leo hariri

AIESEC inajitambulisha kama "jukwaa la kimataifa kwa ajili ya vijana kutafiti na kuendeleza vipaji vyao vya uongozi." [4] Kwa mwaka hutoa nafasi "7700 za uongozi na hufanya mikutano 470 kwa wanachama [wake] ambao ni zaidi ya wanafunzi 80,000". AIESEC pia anaendesha mpango wa kubadilishana wanafunzi kimataifa ambao unawezesha wanafunzi zaidi ya 5550 na wahitimu nafasi ya kuishi na na kutarajali katika nchi nyingine. [4] Ni moja taasisi kubwa duniani inayoongozwa na wanafunzi.

Mwaka 2008 ulihitimisha jubilei ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa AIESEC. Maadhimisho yalifanyika katika mji wa London (Januari 2008), Tokyo (Machi 2008), Budapest (Mei 2008), Bryssel (Juni 2008), Brazili (Agosti 2008), Stockholm (Oktoba 2008), na Marekani (Desemba 2008).

Kudumisha uhusiano wake katika uso wa mabadiliko ya mahusiano ya kimataifa, AIESEC inajipanua katika nchi mpya mara kwa mara, mchakato ambao umeainishwa katika maandishi ya kazi za taasisi hiyo kimataifa. Nchi zilizotajwa kama "Upanuzi maalumu" wa AIESEC mnamo 13 Machi 2009, ni pamoja na Algeria, Angola, Azerbaijan, Bahrain, Benin, Ethiopia, Gabon, Georgia, Ireland, Iran, Mauritius, Mongolia, Oman, Qatar, Ufalme wa Saudi Arabia, Tajikistan, na Vietnam.

Muundo hariri

Kila nchi (wakati mwingine kundi la nchi, au maeneo ndani ya nchi) ambapo AIESEC ipo ina Kamati ya kitaifa y wanachama, ambayo inaratibu shughuli za eneo hilo. Wajumbe pia wanahusika katika Kamati za eneo kwa kila chuo au chuo kikuu.

Mwongozo wa AIESEC hariri

Kama ilivyoelezwa katika tovuti yake, AIESEC inaweka juhudi katika "mabadiliko chanya ya kijamii" na kutumia "Njia ya AIESEC". [5] Njia ya AIESEC inaelezewa kama njia ya kufikia "Amani na utimilifu wa vipaji vya wanadamu." [5] Kulingana na AIESEC, kuna maadili makuu sita, yaani; Kusisimua Uongozi, Kuonyesha Uaminifu, Utofauti wa Maisha, kufurahia Ushiriki, Juhudi za Ubora Ubora na Kafanya kazi endelevu. [5]

Katika ngazi ya mtu binafsi, AIESEC inawezesha wanafunzi kuishi uzoefu wa AIESEC kwa kuchukua nafasi za uongozi, kupata ujuzi wa biashara, na kuujiunganisha na mtandao wa kimataifa wa wanafunzi kwa kuhudhuria mikutano ya kimataifa na kutarajali ng'ambo. Kuna kanuni muhimu tano, yaani Kuchukua Nafasi Imara (lengo kuu: tabia imara), Developing Uelewa binafsi na Upeo binafsi (kuchukua jukumu), Kuongeza Uwezo (kujifunza nadharia na kuitumia katika vitendo), Kujenga Mtandao (mitandao) na changamoto za mtizamo wa kiduniwa(mtizamo wa kidunia kiujumla). [6]

Washirika hariri

Tovuti ya AIESEC anasema kwamba ina ubia wa hadhi na makampuni kadhaa, kati yao ni makampuni kama Alcatel, ABN AMRO, Cadbury Schweppes, DHL, Electrolux, AB InBev, PwC, Enterprise Asia, HP, Microsoft na UBS. Ubia unahusiana hasa na uwepo wa wabia hawa katika vikao vya AIESEC, na utoaji wa vipaji kutoka AIESEC kwenda kwa wabia hawa. [7] AIESEC hutoa chanzo cha vipaji kimataifa kwa AB InBev, Alcatel Lucent, na DHL. [8] [9] [10]

Alumni hariri

Kulingana na tovuti ya Alumni ya AIESEC, watu maarufu kadhaa wamekuwa wanaohusika na taasisi hiyo [11] Nao ni pamoja na:

Wakuu wa Nchi na Serikali


Wafanyabiashara


Wengine

Marejeo hariri

  1. "AIESEC". AIESEC web site. 2009-04. Iliwekwa mnamo 2009-04-06.  Check date values in: |date= (help)
  2. 2.0 2.1 2.2 Kern, Beth (2003-10-02). "AIESEC helps interns make adjustments". University Chronicle. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-01-30. Iliwekwa mnamo 2008-02-11. 
  3. 3.0 3.1 3.2 3.3 "The AIESEC History". AIESEC web site. Iliwekwa mnamo 2008-02-11.  http://www.aiesec.org/cms/aiesec/AI/About/history/index.html Historia ya AIESEC]
  4. 4.0 4.1 "Welcome to AIESEC". AIESEC web site. Iliwekwa mnamo 2008-02-11. 
  5. 5.0 5.1 5.2 "The AIESEC Way". AIESEC web site. Iliwekwa mnamo 2008-02-11. 
  6. "The AIESEC Experience". AIESEC web site. Iliwekwa mnamo 2008-02-11. 
  7. "Global Development Group". AIESEC web site. Iliwekwa mnamo 2008-02-11. 
  8. "AB InBev - AIESEC". AB InBev Website. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-09-08. Iliwekwa mnamo 2009-09-19. 
  9. "Start your journey with us now!". Alcatel Lucent Website. Iliwekwa mnamo 2009-09-19. 
  10. "DHL Global AIESEC Program". DHL Website. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-11-06. Iliwekwa mnamo 2009-09-19. 
  11. "Famous Alumni". AIESEC Alumni International. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-03-26. Iliwekwa mnamo 2009-02-27. 

Viungo vya nje hariri