AIM-9 Sidewinder

AIM-9 Sidewinder ni kombora la masafa mafupi hewa-kwa-hewa, yaani ni kombora ambalo hurushwa kutoka kwenye ndege na inapaswa kugonga ndege nyingine.

AIM-9L sidewinder
AIM-9L sidewinder

Ilianza kutumiwa mwaka wa 1953 ikaingia katika vikosi vya hewa mwaka wa 1956. Ilikuwa inatumika wakati wa vita vya Vietnam sambamba na AIM-7 Sparrow, lakini haikuwa nzuri.