A Grain of Wheat ni riwaya ya tatu na maarufu zaidi ya Ngugi wa Thiong'o, mwandishi kutoka Kenya.

A Grain of Wheat  
Mwandishi (wa){{{mwandishi}}}
ISBNISBN:

Riwaya hii huchanganya hadithi kadhaa pamoja katika hali ya dharura nchini Kenya katika mapambano ya uhuru (1952-1959), unaolenga Mugo aliyekuwa mtulivu, ambaye maisha yake yalitawalwa kwa siri. Hadithi yenyewe inahusu nyumbani kwake katika maandalizi ya kijiji ya sherehe ya siku ya uhuru wa Kenya (siku ya Uhuru). Wapiganaji wa kundi la MAUMAU ambayo ilikuwa ikitumiwa na waafrika kama kundi kuu la kupinga Mkoloni,Mwanajeshi Mkuu R na Koinandu wanapanga tarehe ya kumuua hadharani ikiwa watampata msaliti ambaye aliyemsaliti Kihika (mpiganaji shujaa kutoka kijiji) miaka michache kabla ya Uhuru.

Wahusika hariri

  • Mpweke Mugo, shujaa wa makambi ya Uingereza ambapo yeye aliongoza mgomo wa njaa na yeye pia alijaribu kuzuia mlinzi wa kijiji ili asimpige mwanamke mjamzito hadi kifo. Ingawa yeye hudhaniwa kuwa shujaa katika kitabu chote, yeye ni msaliti wa Kihika aliyemsaliti kwa Waingereza katika tendo la ubinafsi ili kujiokoa.
  • Gikonyo, seremala na mfanyibiashara ambaye ameoa Mumbi. Alikiri kuchukua kiapo cha upinzani wakati wa mkusanyiko katika kambi, alipotolewa mapema alipata kwamba mke wake alikuwa na mtoto pamoja na adui wake Karanja alipokuwa kambini.
  • Mumbi, mke wa Gikonyo na dadake Kihika. Wakati Gikonyo alipokuwa jela mwishowe alazimishwa kulala na Karanja aliyekuwa mkuu wa kijiji maalumu kwa nguvu ya ukoloni kwa njia ya ushirikiano.
  • Karanja, mshirikishi na Waingereza aliyeaminika kuwa msaliti aliyemsaliti Kihika
  • Kihika, mpiganaji wa upinzani ambao waliteka kituo cha polisi na kuwaua Afisa wa Wilaya Robson kabla ya kupatikana na kunyongwa baada ya kusalitiwa na Mugo.
  • John Thompson,mkuu wa utawala wa muingereza anayesimamia eneo la Kikuyu hasa Thabai ni Muingereza anayeshikilia fikira za kiingereza na ana hujumu na kuwadharau waafrika.
 
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu: