Abaloparatide
Abaloparatide, inayouzwa chini ya jina la chapa Tymlos miongoni mwa mengineyo, ni dawa inayotumika kutibu ugonjwa wa mifupa dhaifu (osteoporosis) baada ya kukoma hedhi.[2][1] Kwa wale walio katika hatari kubwa, inaweza kupunguza hatari ya mivunjiko ya mifupa kutoka 5.9% hadi 3.3%.[3] Haipaswi kutumiwa kwa zaidi ya miaka miwili.[2] Inatumika kama sindano chini ya ngozi.[2]
Jina la Utaratibu la (IUPAC) | |
---|---|
L-alanyl-L-valyl-L-seryl-L-α-glutamyl-L-histidyl-L-glutaminyl-L-leucyl-L-leucyl-L-histidyl-L-α-aspartyl-L-lysylglycyl-L-lysyl-L-seryl-L-isoleucyl-L-glutaminyl-L-α-aspartyl-L-leucyl-L-arginyl-L-arginyl-L-arginyl-L-α-glutamyl-L-leucyl-L-leucyl-L-α-glutamyl-L-lysyl-L-leucyl-L-leucyl-2-methylalanyl-L-lysyl-L-leucyl-L-histidyl-L-threonyl-L-alaninamide | |
Data ya kikliniki | |
Majina ya kibiashara | Tymlos, Eladynos[1] |
AHFS/Drugs.com | Monograph |
MedlinePlus | a617038 |
Kategoria ya ujauzito | ? |
Hali ya kisheria | ℞-only (US) |
Njia mbalimbali za matumizi | Sindano ya chini ya ngozi[2] |
Vitambulisho | |
Nambari ya ATC | ? |
Visawe | BA058, BIM-44058 |
Data ya kikemikali | |
Fomyula | C174H299N56O49 |
|
Madhara yake ya kawaida ni mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida, kizunguzungu, kichefuchefu, maumivu ya kichwa, uchovu na maumivu ya sehemu ya juu ya tumbo.[2][3] Matatizo mengine yanayoweza kutokea ni pamoja na ongezeko la hatari ya saratani ya mifupa (osteosarcoma), kalsiamu ya juu ya damu, shinikizo la chini la damu ukiwa umesimama na maumivu kwenye eneo la sindano.[2][3] Ni analogi ya protini inayohusiana na homoni ya parathyroid (PTHrP) na inafanya kazi kwa kukuza ukuaji wa mfupa.[2]
Abaloparatide iliidhinishwa kwa ajii ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2017.[2] Hapo awali ilikataliwa kibali huko Uropa mnamo mwaka wa 2018;[4] hata hivyo, iliidhinishwa baadaye katika mwaka wa 2022.[1] Kufikia mwaka wa 2018, iligharimu takriban dola 1,800 za kwa mwezi nchini Marekani.[3] Kufikia mwaka wa 2019 haijulikani jinsi ufanisi wake ikilinganishwa na bisphosphonates za bei ya chini.[3]
Marejeleo
hariri- ↑ 1.0 1.1 1.2 "Eladynos". European Medicines Agency (kwa Kiingereza). 12 Oktoba 2022. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 3 Machi 2021. Iliwekwa mnamo 6 Oktoba 2023.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 2.5 2.6 2.7 Hitilafu ya kutaja: Invalid
<ref>
tag; no text was provided for refs namedAHFS2021
- ↑ 3.0 3.1 3.2 3.3 3.4 Hitilafu ya kutaja: Invalid
<ref>
tag; no text was provided for refs namedBen2019
- ↑ "Eladynos". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 3 Machi 2021. Iliwekwa mnamo 17 Julai 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)