Abciximab, inayouzwa kwa jina la biashara Reopro, ni dawa iliyotumiwa wakati wa Upasuaji wa moyo bila kufungua kifua (percutaneous coronary angioplasty).[1] Dawa hii inatolewa kwa njia ya sindano kwenye mshipa.[1] Mwanzo wake kamili hutokea ndani ya dakika 10 na hudumu hadi masaa 48 baada ya kusimamishwa.[1]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kutokwa na damu, shinikizo la chini la damu, kichefuchefu, maumivu ya kichwa na uvimbe wa pembeni.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha mzio mkali unaoweza kutishia maisha (anaphylaxis) na chembe za damu za pletleti za chini.[1] Usalama wa matumizi yake katika ujauzito hauko wazi.[1] Dawa hii ni kizuizi cha glycoprotein_IIb/IIIa ambacho hufanya kazi kwa kuzuia chembe za damu pletleti kushikamana pamoja.[1]

Abciximab iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 1994.[1] Nchini Marekani, miligramu 10 hugharimu takriban dola 1,300 za Marekani kufikia mwaka wa 2022.[2]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 1.7 "Abciximab Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 4 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 13 Januari 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "ReoPro Prices, Coupons & Patient Assistance Programs". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 10 Februari 2018. Iliwekwa mnamo 13 Januari 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Abciximab kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.