Acalabrutinib, inayouzwa kwa jina la chapa Calquence, ni dawa inayotumika kutibu lymphoma ya seli ya mshipa (MCL) na leukemia sugu ya lymphocytic (CLL).[1][2] Kwa CLL inaweza kutumika mwanzoni au kwa wale ambao wameshindwa matibabu mengine.[2] Inachukuliwa kwa mdomo.[3]

Jina la Utaratibu la (IUPAC)
4-{8-Amino-3-[(2S)-1-(2-butynoyl)-2-pyrrolidinyl]imidazo[1,5-a]pyrazin-1-yl}-N-(2-pyridinyl)benzamide
Data ya kikliniki
Majina ya kibiashara Calquence
AHFS/Drugs.com Monograph
MedlinePlus a618004
Taarifa za leseni US Daily Med:link
Kategoria ya ujauzito C(AU) ?(US)
Hali ya kisheria Prescription Only (S4) (AU) -only (US)
Njia mbalimbali za matumizi Kwa mdomo
Vitambulisho
Nambari ya ATC ?
Visawe ACP-196
Data ya kikemikali
Fomyula C26H23N7O2 

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kuumwa na kichwa, kuhisi uchovu, chembechembe nyekundu za damu kupungua, chembechembe nyeupe za damu kidogo na chembechembe za kugandisha damu kidogo.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha maambukizi, kutokwa na damu, saratani zaidi, na mpapatiko wa atiria.[3] Matumizi yake wakati wa ujauzito yanaweza kumdhuru mtoto.[3] Ni kizuizi cha tyrosine kinase cha Bruton, ambacho hupunguza kasi ya mkusanyiko wa seli za B za saratani.[2]

Acalabrutinib iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2017 na Ulaya mwaka wa 2020.[1][2] Nchini Uingereza, mwezi mmoja wa dawa hii uligharimu NHS takriban £5,100 kufikia mwaka wa 2021.[4] Kiasi hiki nchini Marekani ni takriban dola 15,000 za Marekani.[5]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 "Acalabrutinib Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 4 Novemba 2019. Iliwekwa mnamo 16 Machi 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 "Calquence EPAR". European Medicines Agency. 20 Julai 2020. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 17 Novemba 2020. Iliwekwa mnamo 11 Novemba 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) Text was copied from this source which is © European Medicines Agency. Reproduction is authorized provided the source is acknowledged.
  3. 3.0 3.1 3.2 "Calquence- acalabrutinib capsule, gelatin coated". DailyMed. 22 Novemba 2019. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 23 Machi 2021. Iliwekwa mnamo 11 Novemba 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. BNF 81: March-September 2021. BMJ Group and the Pharmaceutical Press. 2021. uk. 1010. ISBN 978-0857114105.
  5. "Calquence Prices, Coupons & Patient Assistance Programs". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 18 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 13 Januari 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)