Acamprosate
Acamprosate, inayouzwa kwa jina la chapa Campral miongoni mwa mengine, ni dawa inayotumiwa pamoja na ushauri nasaha kutibu utegemezi wa pombe.[1] Inapotumiwa peke yake, haina ufanisi kwa watu wengi;[3] inafanya kazi vyema zaidi inapotumiwa pamoja na ushauri nasaha.[1][4] Inachukuliwa kwa mdomo.[5]
Jina la Utaratibu la (IUPAC) | |
---|---|
3-Acetamidopropane-1-sulfonic acid | |
Data ya kikliniki | |
Majina ya kibiashara | Campral, Aotal, mengineyo[1] |
AHFS/Drugs.com | Monograph |
Kategoria ya ujauzito | C[2] (US) B2 (AU) |
Hali ya kisheria | Prescription Only (S4) (AU) POM (UK) ℞-only (US) |
Njia mbalimbali za matumizi | Kwa mdomo[2] |
Data ya utendakazi | |
Uingiaji katika mzunguko wa mwili | 11%[2] |
Kufunga kwa protini | Kunapuuzika[2] |
Kimetaboliki | Hakuna[2] |
Nusu uhai | Masaa 20 hadi 33 [2] |
Utoaji wa uchafu | Figo[2] |
Vitambulisho | |
Nambari ya ATC | ? |
Visawe | N-Acetyl homotaurine |
Data ya kikemikali | |
Fomyula | C5H11NO4S |
| |
(hii ni nini?) (thibitisha) |
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kuhara na udhaifu.[6] Madhara yake makubwa yanaweza kujumuisha athari za mzio, mabadiliko ya hisia, mawazo ya kujiua na mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida.[7] Kiwango cha chini kinapendekezwa kwa watu walio na matatizo madogo ya figo na matumizi yake hayapendekezi kwa watu wenye ugonjwa mkali wa figo.[6] Matumizi yake ni sawa katika hali ya kutofanya kazi kwa ini kwa chini hadi wastani.[8] Usalama wake wakati wa ujauzito haueleweki.[9] Acamprosate inadhaniwa kufanya kazi kwa kubadilisha ishara za kemikali kwenye ubongo.[8]
Acamprosate iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2004[6] na iko kwenye Orodha ya Dawa Muhimu ya Shirika la Afya Ulimwenguni.[10] Inapatikana kama dawa ya kawaida nchini Uingereza ambapo mwezi mmoja wa matumizi yake uligharimu NHS kama pauni 30 kufikia mwaka wa 2020.[5] Kiasi hiki nchini Marekani kiligharimu kama dola 80 za Marekani kufikia mwaka wa 2020.[11]
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 1.2 Plosker, GL (Julai 2015). "Acamprosate: A Review of Its Use in Alcohol Dependence". Drugs. 75 (11): 1255–68. doi:10.1007/s40265-015-0423-9. PMID 26084940.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 2.5 2.6 "Campral label" (PDF). FDA. Januari 2012. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka (PDF) kutoka chanzo mnamo 27 Februari 2017. Iliwekwa mnamo 27 Novemba 2017.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) For label updates see FDA index page for NDA 021431 Archived 2021-08-27 at the Wayback Machine - ↑ Malenka RC, Nestler EJ, Hyman SE, Holtzman DM (2015). "Chapter 16: Reinforcement and Addictive Disorders". Molecular Neuropharmacology: A Foundation for Clinical Neuroscience (tol. la 3rd). New York: McGraw-Hill Medical. ISBN 9780071827706.
Unfortunately, acamprosate is not adequately effective for most alcoholics.
- ↑ Nutt, DJ (2014). "Doing it by numbers: A simple approach to reducing the harms of alcohol". Journal of Psychopharmacology. 28 (1): 3–7. doi:10.1177/0269881113512038. PMID 24399337. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-08-27. Iliwekwa mnamo 2020-01-22.
- ↑ 5.0 5.1 BNF 79 : March 2020. London: Royal Pharmaceutical Society. 2020. uk. 509. ISBN 9780857113658.
- ↑ 6.0 6.1 6.2 "Acamprosate Calcium Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 4 Novemba 2019. Iliwekwa mnamo 7 Oktoba 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Acamprosate". drugs.com. 2005-03-25. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 22 Desemba 2006. Iliwekwa mnamo 2007-01-08.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 8.0 8.1 Williams, SH. (2005). "Medications for treating alcohol dependence". American Family Physician. 72 (9): 1775–1780. PMID 16300039. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-09-29. Iliwekwa mnamo 2006-11-29.
- ↑ "Acamprosate (Campral) Use During Pregnancy". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 Novemba 2020. Iliwekwa mnamo 7 Oktoba 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ World Health Organization (2023). The selection and use of essential medicines 2023: web annex A: World Health Organization model list of essential medicines: 23rd list (2023). Geneva: World Health Organization. hdl:10665/371090. WHO/MHP/HPS/EML/2023.02.
- ↑ "Acamprosate Prices, Coupons & Savings Tips". GoodRx (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 26 Septemba 2016. Iliwekwa mnamo 7 Oktoba 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)