Acetylcysteine, pia inajulikana kama N-acetylcysteine (NAC), ni dawa ambayo hutumiwa kutibu kuzidiwa na dozi ya paracetamol (acetaminophen), na kulegeza kamasi nene kwa watu walio na uvimbe wa fibrosisi au ugonjwa sugu wa mapafu.[3] Inaweza kuchukuliwa kwa njia ya mshipa, kwa mdomo, au kwa kuvuta pumzi kama ukungu.[3] Baadhi ya watu huitumia kama virutubisho vya lishe.[6][7]

Jina la (IUPAC)
(2R)-2-acetamido-3-sulfanylpropanoic acid[1]
Data ya kikliniki
Majina ya kibiashara Acetadote, Fluimucil, Mucomyst, mengineyo
AHFS/Drugs.com Monograph
Taarifa za leseni US Daily Med:link
Kategoria ya ujauzito B2(AU) B(US)
Hali ya kisheria Pharmacy Only (S2) (AU) OTC (US)
Njia mbalimbali za matumizi kwa mdomo, sindano, kwa kuvuta pumzi
Data ya utendakazi
Uingiaji katika mzunguko wa mwili 10% (kwa mdomo)[2]
Kufunga kwa protini 50 hadi 83%[3]
Kimetaboliki Ini[3]
Nusu uhai Masaa 5.6 [4]
Utoaji wa uchafu Figo (30%),[3] kinyesi (3%)
Vitambulisho
Nambari ya ATC ?
Visawe N-acetylcysteine; N-acetyl-L-cysteine; NALC; NAC
Data ya kikemikali
Fomyula C5H9NO3S 
Massi ya molekuli 163.195
Data ya kimwili
Kiwango cha kuyeyuka 109–110 °C (228–230 °F) [5]
Spec. rot +5° (c = 3% ndani ya maji)[5]
 YesY(Hiki ni nini?)  (thibitisha)

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kichefuchefu na kutapika wakati inachukuliwa kwa mdomo.[3] Ngozi mara kwa mara inaweza kuwa nyekundu na kuwasha kwa namna yoyote ile.[3] Aina isiyo ya kinga ya anaphylaxis inaweza pia kutokea.[3] Inaonekana kuwa salama wakati wa ujauzito.[3] Katika hali ya kuzidiwa na dozi ya paracetamol, inafanya kazi kwa kuongeza kiwango cha glutathione, antioxidant ambayo inaweza kupunguza bidhaa za sumu zinazotokana na mchakato wa kuvunjika kwa paracetamol.[3] Inapovutwa kwa pumzi, hufanya kama mucolytic kwa kupunguza unene wa kamasi.[8]

Acetylcysteine ilipewa hati miliki awali katika mwaka wa 1960 na ikaanza kutumika kimatibabu katika mwaka wa 1968.[9] Iko kwenye Orodha ya Dawa Muhimu ya Shirika la Afya Ulimwenguni.[10] Inapatikana kama dawa ya kawaida na ni ya bei nafuu.[11] Mwongozo juu ya matumizi yake hutofautiana kati ya nchi.[11]

Marejeo

hariri
  1. "L-Cysteine, N-acetyl- - Compound Summary". PubChem Compound. USA: National Center for Biotechnology Information. 25 Machi 2005. Identification. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 12 Januari 2014. Iliwekwa mnamo 9 Januari 2012.
  2. Stockley, Robert A. (2008). Chronic Obstructive Pulmonary Disease a Practical Guide to Management. Chichester: John Wiley & Sons. uk. 750. ISBN 9780470755280. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 8 Septemba 2017.
  3. 3.00 3.01 3.02 3.03 3.04 3.05 3.06 3.07 3.08 3.09 "Acetylcysteine". The American Society of Health-System Pharmacists. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 23 Septemba 2015. Iliwekwa mnamo 22 Ago 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "ACETADOTE (acetylcysteine) injection, solution [Cumberland Pharmaceuticals Inc.]". DailyMed. Cumberland Pharmaceuticals Inc. Juni 2013. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 13 Januari 2014. Iliwekwa mnamo 8 Novemba 2013.
  5. 5.0 5.1 "N-ACETYL-L-CYSTEINE Product Information" (PDF). Sigma. Sigma-aldrich. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 11 Juni 2014. Iliwekwa mnamo 9 Novemba 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. Talbott, Shawn M. (2012). A Guide to Understanding Dietary Supplements (kwa Kiingereza). Routledge. uk. 469. ISBN 9781136805707. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 8 Septemba 2017.
  7. "Cysteine". University of Maryland Medical Center (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 1 Julai 2017. Iliwekwa mnamo 23 Juni 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. Sadowska, Anna M; Verbraecken, J; Darquennes, K; De Backer, WA (Desemba 2006). "Role of N-acetylcysteine in the management of COPD". International Journal of Chronic Obstructive Pulmonary Disease. 1 (4): 425–434. doi:10.2147/copd.2006.1.4.425. ISSN 1176-9106. PMC 2707813. PMID 18044098.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unflagged free DOI (link)
  9. Fischer, János; Ganellin, C. Robin (2006). Analogue-Based Drug Discovery. Weinheim: Wiley-VCH. uk. 544. ISBN 9783527607495. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 8 Septemba 2017.
  10. World Health Organization (2019). World Health Organization model list of essential medicines: 21st list 2019. Geneva: World Health Organization. hdl:10665/325771. WHO/MVP/EMP/IAU/2019.06. License: CC BY-NC-SA 3.0 IGO.
  11. 11.0 11.1 Hitchings, Andrew; Lonsdale, Dagan; Burrage, Daniel; Baker, Emma (2019). The Top 100 Drugs: Clinical Pharmacology and Practical Prescribing (kwa Kiingereza) (tol. la 2nd). Elsevier. ku. 30–31. ISBN 978-0-7020-7442-4. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 22 Mei 2021. Iliwekwa mnamo 9 Novemba 2021.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)