Adriano Celentano (alizaliwa Milano, 6 Januari 1938) ni mwimbaji, mtunzi wa nyimbo, mwanamuziki, mwigizaji na mkurugenzi wa filamu kutoka nchini Italia.

Adriano Celentano (2013)

Kwao anajulikana kama " il Molleggiato ", yaani "mnyumbufu" kutokana na namna yake ya kucheza dansi. [1] [2]

Mnamo 1962, Celentano alianzisha lebo ya rekodi Clan Celentano. Kazi zake zinazojulikana zaidi ni " 24.000 Baci ", " Il Tuo Bacio e' Come un Rock " na " Si e' Spento il Sole ".

Marejeo hariri