Aga Khan (Kifarsi: آقا خان) ni cheo cha imamu au kiongozi wa Wanizari ambao ni kundi kubwa la pili ndani ya Waislamu Washia wakihesabiwa katika dhehebu la Waismaili.

Aga Khan wa sasa,Shah Karim Al Hussein

Maimamu wa Wanizari walianza kutumia cheo cha Aga Khan wakati wa karne ya 19 ambako Hasan Ali Shah aliyehesabiwa kama imamu wa 46 wa Kiismaili alipewa cheo hiki na mfalme au shah wa Uajemi.

MaAga Khan hadi sasa ni wafuatao:

  1. Aga Khan I - Hasan Ali Shah Mehalatee (1800–1881), Imamu wa 46 wa Kiismaili (1817–1881)
  2. Aga Khan II - Ali Shah (~1830–1885), Imamu wa 47 wa Kiismaili (12 Aprili 1881–1885)
  3. Aga Khan III - Prince Sultan Mohammed, (1877–1957), Imamu wa 48 wa Kiismaili (17 Agosti 1885–1957)
  4. Aga Khan IV - Prince Karim Al Husseini (b. 1936),Imamu wa 49 wa Kiismaili (tangu 11 Julai 1957)
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.