Agano ni neno lenye maana nzito katika dini mbalimbali, hasa zile zinazofuata imani ya Abrahamu kwa Mungu mmoja.

Amri Kumi zilivyoandikwa mbele ya ikulu ya Texas, Marekani.

Upekee wake ni kwamba agano hilo si kati ya pande mbili zilizo sawa, kama yale kati ya watu, bali ni Mungu anayelianzisha na kupanga masharti, akimhimiza binadamu kukubali na kuwa mwaminifu.

Jina hariri

Agano ni tafsiri ya kawaida ya neno la Kiebrania ברית, bərîṯ au berith.

Katika Biblia ya Kiebrania linatumika mara 264.[1]

Tafsiri ya Kigiriki katika Septuaginta na katika Agano Jipya ni διαθήκη, diatheke,[2] ambalo lina maana ya wasia pia (ndiyo sababu katika Kilatini tunakuta Testamentum).

Uyahudi hariri

Wazo la agano ni la msingi kwa Wayahudi, nao wanaona lile alilofanya Mungu na Musa kwenye mlima Sinai linawahusu wao, wakati kwa mataifa mengine lipo lile alilolifanya na Noah. [3]

Ukristo hariri

Ukristo unakiri kwamba Mungu alifanya maagano mengine na binadamu, lakini hatimaye alianzisha "Agano Jipya" na la milele katika damu ya Yesu Kristo iliyomwagwa kwa ondoleo la dhambi za watu wote watakaomuamini.[4]

Uislamu hariri

Uislamu unaendeleza imani katika agano la Mungu na Abrahamu, ambalo tohara ni ishara yake ya nje.

Tanbihi hariri

  1. [1]
  2. The Blue Letter Bible, Strong's G1242.. Jalada kutoka ya awali juu ya 2012-07-28. Iliwekwa mnamo 2015-11-03.
  3. "...Judaism does not deny salvation to those outside of its fold, for, according to Jewish law, all non-Jews who observe the Noahide laws will participate in salvation and in the rewards of the world to come". The Torah, W. G. Plaut, Union of American Hebrew Congregations, New York, 1981; p. 71.
  4. Grudem, Wayne A. "The Covenants Between God and Man." Systematic Theology: an Introduction to Biblical Doctrine. Grand Rapids, MI: Zondervan, 2000. 515. Print.
  Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.