Akachi Adimora-Ezeigbo
Akachi Adimora-Ezeigbo ni mwandishi na mwalimu kutoka Nigeria, ambaye kazi zake zilizochapishwa ni pamoja na riwaya, mashairi, hadithi fupi, vitabu kwa watoto, makala, na uandishi wa habari.[1] Ameshinda tuzo kadhaa nchini Nigeria, ikiwa ni pamoja na Tuzo ya Nigeria kwa Fasihi.[2]
Wasifu
haririAkachi Adimora-Ezeigbo alizaliwa na kukulia Mashariki mwa Nigeria, lakini sasa anaishi Lagos. Yeye ni mtoto wa kwanza wa Joshua na Christiana Adimora na ana ndugu watano. Alikulia sehemu kwa sehemu katika mazingira ya vijijini na sehemu katika mji, na anachanganya mambo haya mawili kama historia na mazingira kwa hadithi zake za watoto na fasihi ya watu wazima. Ingawa alizaliwa Mashariki mwa Nigeria, ameishi katika sehemu tofauti za nchi - Mashariki, Kaskazini, na Magharibi. Amesafiri sana Afrika, Ulaya, na Marekani.
Alihitimu Shahada ya Sanaa (BA) na Shahada ya Uzamili (MA) katika Kiingereza kutoka Chuo Kikuu cha Lagos na Shahada ya Uzamivu (Ph.D.) kutoka Chuo Kikuu cha Ibadan, Nigeria. Pia ana Stashahada ya Uzamili katika Elimu (PGDE) kutoka Chuo Kikuu cha Lagos.
Kama mkufunzi, mwandishi, mwandishi wa riwaya, mchambuzi, mwanazuoni, mwandishi wa makala, mwandishi wa habari, na msimamizi, aliteuliwa kuwa Profesa wa Kiingereza katika Chuo Kikuu cha Lagos mnamo 1999. Amefundisha katika chuo kikuu hiki, katika Idara ya Kiingereza, tangu mwaka 1981. Alikuwa mkuu wa Idara ya Kiingereza mwaka 1997 na 1998, kuanzia mwaka 2002 hadi 2005, na 2008-2009. Mnamo Septemba 2015, alihama kwenda Chuo Kikuu cha Ndufu-Alike, Ikwo, Jimbo la Ebonyi, Kusini-Mashariki mwa Nigeria, ambapo ameendelea kufundisha wanafunzi na kuwa mwongozi kwa wakufunzi wadogo.
Yeye ni mke wa Profesa Chris Ezeigbo na wana watoto watatu.
Marejeo
hariri- ↑ "Interview with Nigerian Writer, Akachi Adimora-Ezeigbo". Geosi Reads (kwa Kiingereza). 2013-08-22. Iliwekwa mnamo 2024-05-03.
- ↑ "African Books Collective: Akachi Adimora-Ezeigbo". www.africanbookscollective.com. Iliwekwa mnamo 2024-05-03.
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Akachi Adimora-Ezeigbo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |