Aktini (actinium) ni elementi ya kikemia yenye namba atomia 89 na alama ya Ac . Uzani atomia wa Aktini ni 227.

Aktini (Aktinium)
Jina la Elementi Aktini (Aktinium)
Alama Ac
Namba atomia 89
Mfululizo safu (haijulikani)
Uzani atomia 227
Valensi 2, 8, 18, 32, 18, 9, 2
Densiti 10 g/cm³ (kadirio)
Ugumu (Mohs) -
Asilimia za ganda la dunia 0 % (haba mno)
Hali maada mango
Mengineyo nururifu

Aktini ni metali yenye rangi ya fedha. Ni nururifu kiasi cha kung'aa kwenye giza. Hata kiwango kidogo cha aktini ni hatari kwa afya ya watu. Isotopi zake huwa na nusumaisha ya siku chache, isipokuwa 227Ac, inayotokea kiasili katika madini ya urani, ina nusumaisha ya miaka 21.8.

Aktini iligunduliwa mnamo 1899 na Mfaransa André-Louis Debierne. Mnamo 1899, Debierne alielezea dutu hii kuwa inafanana na titani [1] na pia na thori . [2]

Marejeo

hariri
  1. Debierne, André-Louis (1899). "Sur un nouvelle matière radio-active". Comptes rendus (kwa French). 129: 593–595.{{cite journal}}: CS1 maint: unrecognized language (link)
  2. Debierne, André-Louis (1900–1901). "Sur un nouvelle matière radio-actif – l'actinium". Comptes rendus (kwa French). 130: 906–908.{{cite journal}}: CS1 maint: unrecognized language (link)
  Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Aktini kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.