Albert Szent-Györgyi
Albert Szent-Györgyi (16 Septemba 1893 – 22 Oktoba 1986) alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Hungaria. Pamoja na nchi yake ya kuzaliwa alifanya kazi katika nchi mbalimbali kama Uholanzi, Ujerumani, Uingereza na Marekani. Alichunguza mambo mengi ya biokemia, na anajulikana hasa kwa utafiti wake wa vitamini C. Mwaka wa 1937 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba.
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Albert Szent-Györgyi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |