Alexandra Boltasseva

Alexandra Boltasseva ni profesa wa uhandisi wa umeme na kompyuta kutoka Chuo Kikuu cha Purdue, [1] pia ni mhariri mkuu wa jarida la The Optical Society 's Optical Materials Express . [2] Utafiti wake unaangazia matirio za plasmonic, mchanganyiko wa metali zilizoundwa na mwanadamu ambazo hutumia plasmoni kufikia sifa za macho ambazo hazionekani katika macho ya kawaida. [3]

Elimu na Kazi hariri

Boltasseva alisomea shahada uzamili na shahada ya uzamivu katika fizikia katika Taasisi ya Fizikia na Teknolojia ya Moscow, akikamilisha miradi yake ya utafiti juu ya leza za visima vya quantum katika Taasisi ya Lebedev Physical Institute . Alihamia Chuo Kikuu cha Ufundi cha Denmark kwa masomo yake ya udhamivu katika nanophotonics na nanofabrication, akifanya kazi na Sergey I. Bozhevolnyi . [4] Kufuatia PhD yake, Boltasseva alifanya kazi katika kampuni mbili za upigaji picha kabla ya kurudi katika Chuo Kikuu cha Ufundi cha Denmark kama postdoc na baadaye profesa msaidizi. Mnamo 2008 alihamia Chuo Kikuu cha Purdue na kwa sasa ni Profesa wa Ron And Dotty Garvin Tonjes wa Uhandisi wa Umeme na Kompyuta, [5] vile vile ana tuzo za heshima katika Uhandisi wa Vifaa. [6]

Marejeo hariri

  1. "Alexandra Boltasseva - Materials Engineering". Materials Engineering - Purdue University (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-08-17. 
  2. "OSA Publishing Announces New Editors-in-Chief for Three Journals". CNBC. Iliwekwa mnamo 2016-01-07. 
  3. Krieger, Kim (2012-04-25). "Metamaterials Step Into the Light". IEEE Spectrum: Technology, Engineering, and Science News (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-04-05. 
  4. "Interview with Prof. Alexandra Boltasseva". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-11-02. Iliwekwa mnamo 18 September 2019.  Check date values in: |accessdate= (help)
  5. "ECE faculty appointed to named professorships". Electrical and Computer Engineering - Purdue University (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-08-17. 
  6. "Alexandra Boltasseva - Materials Engineering". Materials Engineering - Purdue University (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-08-17. "Alexandra Boltasseva - Materials Engineering".
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Alexandra Boltasseva kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.