Ali Farka Touré ni mmoja wa wanamuziki mahiri barani Afrika. Alizaliwa jijini Bamako nchini Mali mwaka 1939. Jina lake hasa ni Ali Ibrahim Touré. Muziki wa Ali Farka Touré ni mchanganyiko wa muziki wa asili wa Mali na muziki wa Amerika ya Kaskazini hasa blues.

Ali Farka Toure

Touré alizaliwa katika kijiji cha Kanau katika ukingo wa mto Niger, kaskazini magharibi mwa nchi ya Mali. Mama yake alikuwa na watoto kumi ambapo ndugu zake wote walifariki wakiwa wachanga. Jina la "Farka" ni jina la utani ambalo alipewa na wazazi wake likimaanisha mnyama punda kutokana na kuwa na msimamo mkali na kiburi.

Muziki wa Touré una nguvu kama za miujiza. Wapenzi wake dunia nzima wamelogwa na upigaji wake wa gitaa. Mara nyingi nyimbo zake amekuwa akiimba kwa lugha za Kisonghai, Kifula, na Kitamasheck. Albamu yake iitwayo Talking Timbukuta, ambayo aliitoa kwa kushirikiana na mwanamuziki Ry Cooder, iliuzwa na kumpatia umaarufu mkubwa hasa katika soko la muziki la nchi za Magharibi. Mwaka 2005 alitoa albamu ya In the Heart of the Moon akishirikiana na mwanamuziki Toumani Diabaté. Albamu hii ilimpatia tuzo ya Grammy.

Pamoja na muziki, Ali Farka Touré alikuwa akijihusisha na masuala ya kisiasa. Mwaka 2004 alichaguliwa kuwa meya wa mji wa Niafunké.

Ali Farka Touré alifariki dunia 7 Machi 2006 baada ya kuugua ugonjwa wa kansa.

Albamu

hariri
  • 1976 - Farka
  • 1987 - Ali Farka Touré
  • 1990 - The River (World Circuit)
  • 1992 - The Source (World Circuit)
  • 1994 - Talking Timbuktu (World Circuit)
  • 1996 - Radio Mali (World Circuit)
  • 1999 - Niafunké (World Circuit)
  • 2004 - Red/Green - 2004 (World Circuit; remastered original albums from 1979 and 1988)
  • 2005 - In The Heart Of The Moon

Filamu

hariri

Viungo vya nje

hariri