Alter ego
Alter ego (kutoka Kilatini, "mwingine wake") ni kama nafsi nyingine ya pili ndani ya mtu mwenyewe.
Kwa mfano, kwenye The Strange Case of Dr Jekyll and Mr Hyde, Mr. Hyde alikuwa alter ego mwovu wa Dr. Jekyll (walikuwa mtu yuleyule, lakini wenye tofauti ya hali za kinafsi).
Istilahi hii pia hutumika kwenye bunilizi maarufu, kama vile vitabu vya hadithi za picha na vitendo, sura au umbo la siri la shujaa wa ajabu, sungusungu au mpinga uhalifu:
- Superman alter ego yake ni Clark Kent
- Batman alter ego yake ni Bruce Wayne
- Spider-Man alter ego yake ni Peter Parker
Pia wakati mwingine msanii anatumia alter ego, kama:
- Ziggy Stardust alikuwa alter ego wa David Bowie
- Marilyn Manson ni jina la kisanii la Brian Warner