Alton Edwards ni mwimbaji wa Zimbabwe, ambaye alikuwa na wimbo uliokuwa kwenye chati ya nyimbo bora 20 zilizosikilizwa sana nchini Uingereza. Nyimbo hiyo ili julikana kwa jina la "I Just Wanna (Spend Some Time with You)" mnamo Januari, mwaka1982. [1] [2] Aliandika na kurekodi wimbo uitwao "Thank You from Africa" ambao ulikuwa wimbo wa kuwashukuru wasanii wa magharibi kwa msaada waliopewa Afrika, haswa Ethiopia . Wimbo huo bado unachezwa kwenye TV ya Zimbabwe na baadhi ya nchi nyingine za Afrika. Mapato yote yalikusanywa na Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu .

Edwards ni mjomba wa Warren Mills ambaye alikuwa na nyimbo kama vile "Mickey's Monkey" na "Sunshine" kwenye rekodi lebo ya Zomba / Jive Records . Mills pia ni binamu wa Rozalla, ambaye alikuwa na vibao kama "Everybody's Free" na "Are You Ready to Fly". Edwards bado ni mwimbaji anayefanya kazi kwenye muziki wa Uingereza. Anafanya kazi mara kwa mara na Angelo Starr (kaka wa Edwin Starr ) na Alexander O'Neal .

Marejeo

hariri
  1. "Alton Edwards - Biography & History". AllMusic. Iliwekwa mnamo 28 Januari 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Zimbabwean musicians Alton Edwards and Alistair Abrahams in court over Will despute". Zimbabwe News. 20 Septemba 2017. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 29 Januari 2018. Iliwekwa mnamo 28 Januari 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)