Altretamini
Altretamini (Altretamine), inayouzwa kwa jina la chapa Hexalen, ni dawa inayotumika kutibu saratani ya ovari.[1] Hasa hutumiwa kutibu ugonjwa wa hali ya juu wakati matibabu mengine hayafanyi kazi.[1] Dawa hii inachukuliwa kwa mdomo.[1]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kichefuchefu, kutapika, kuhara, kupoteza nywele, kuzuia mno uzlishaji wa uboho wa mfupa, matatizo ya mishipa ya pembeni na upele.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha matatizo ya kihisia na saratani ya kiwango cha juu.[2] Matumizi yake wakati wa ujauzito yanaweza kumdhuru mtoto.[2] Dawa hii ni ajenti inayoathiriana na atomu zenye elektroni nyingi ili kuunda kifungo shirikishi (alkylating agent).[1]
Altretamini iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 1990.[1] Kufikia mwaka wa 2022 haijakuwa ikipatikana kibiashara nchini Marekani.[3]
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 "Altretamine". LiverTox: Clinical and Research Information on Drug-Induced Liver Injury. National Institute of Diabetes and Digestive and Kidney Diseases. 2012. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 6 Mei 2021. Iliwekwa mnamo 14 Januari 2022.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 2.0 2.1 "Altretamine Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 26 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 14 Januari 2022.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Drugs@FDA: FDA-Approved Drugs". www.accessdata.fda.gov. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 27 Agosti 2021. Iliwekwa mnamo 14 Januari 2022.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Altretamini kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |