Alumni ni neno la kutaja watu waliokuwa wanafunzi wa chuo kikuu fulani. Asili ya neno ni lugha ya Kilatini ni uwingi wa alumnus inayomaanisha "anayelelewa, anayelishwa".

Desturi ya kuunda umoja wa wanafunzi wa kale wachuo fulani ilianzishwa huko Marekani kwa shabaha ya kupata msaada wa watu wenye kazi njema na mapato mema walio tayari kusaidia chuo chao cha zamani. Alumni wanajitolea kwa hali na mali, kwa kukipa chuo chao pesa, kwa kutumia athira yao katika siasa kwa ajili ya sheria za kusaidia elimu, kwa kuwapa wanafunzi wachuo chao nafasi za ajira na kadhalika.

Siku hizi kuna vyama vingi vya alumni