Alvimopani (Alvimopan), inayouzwa chini ya jina la chapa Entereg, ni dawa inayotumika kuharakisha kupona kutokana na ugonjwa wa ileus baada ya kupasuliwa kusiko kamili kwa sehemu ya matumbo kupitia njia ya anastomosisi ya upasuaji.[1] Dawa hii inaweza kutumika baada ya upasuaji wa utumbo mdogo au utumbo mkubwa.[2] Inachukuliwa kwa mdomo.[2]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kiungulia.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha mshtuko wa moyo na potasiamu ya chini.[1][2] Usalama wa matumizi yake katika ujauzito hauko wazi.[3] Ni mpinzani wa kipokezi cha μ-opioid kinaychofanya kazi kwa pembeni.[2]

Alvimopani iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2008.[1] Nchini Marekani, dozi 15 za miligramu 12 hugharimu takriban Dola 2,900 kufikia mwaka wa 2022.[4]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 "DailyMed - ALVIMOPAN capsule". dailymed.nlm.nih.gov. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 19 Aprili 2021. Iliwekwa mnamo 14 Januari 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 "Alvimopan Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 Juni 2021. Iliwekwa mnamo 14 Januari 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Alvimopan (Entereg) Use During Pregnancy". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 3 Desemba 2020. Iliwekwa mnamo 14 Januari 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Entereg Prices, Coupons & Patient Assistance Programs". Drugs.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 14 Januari 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Alvimopani kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.